Boniface Mwangi asherehekea miaka 14 katika ndoa

Muhtasari

• Mwanaharakati wa haki za kibinadamu Boniface Mwangi na mkewe wamesherehekea miaka 14 katika ndoa.

• Mwangi anasema kwamba anahisi mtu mwenye kubarikiwa kwa sababu mkewe yuko katika maisha yake.

Bonface Mwangi na Mkewe Njeri
Image: Boniface Mwqangi (Facebook)

Mwanaharakati wa haki za kibinadamu Boniface Mwangi alimsherehekea mkewe kwa jumbe za mahanjumati Jumanne siku ya kusherehekea wakawake duniani, ambayo pia ndio tarehe walifunga ndoa miaka zaidi ya kumi iliyopita.

Mwangi ambaye hajawahi yaficha mapenzi yake kwa mkewe Njeri alisema kwamba walijuana miaka kumi na sita iliyopita na sasa wamedumu katika ndoa kwa miaka kumi na minne.

Katika mahojiano ya kipekee muda fulani nyuma, Mwangi alifichua kwamba mkewe pia ni mwanaharakati na mapenzi yao yaliota wakiwa katika harakati za maandamano jijini Nairobi dhidi ya unyanyasaji wa polisi kwa raia wasio na hatia miaka miaka 16 iliyopita.

“Nimemjua huyu mwanamke wa kipekee kwa miaka 16. Leo, miaka 14 iliyopita tulifunga ndoa. Mimi ni mtu wa maana sana sasa kwa sababu Njeri yupo katika maisha yangu.” Mwangi aliandika.

Vile vile mwanaharakati huyo alimsifia mkewe kwa kusimama upande wa Faraja yake siku zote ambazo dunia mzima ilionekana kumsonya. Alisema kwamba angepewa nafasi nyingine tena ya kufanya chaguo bora la mtu wa kukaa naye maishani basi asingekosea tena kuchagua Njeri.

“Kama ningekuwa nianze maisha upya tena, ningemuoa Njeri tena. Najua Mungu ananipenda na ndio maana aliumba Njeri kwa ajili yangu. Nampenda zaidi ya maelezo.” Aliandika Mwangi.

Mwangi ambaye alishinda zawadi ya picha bora kutoka kwa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007/08 awali katika mahojiano aliwahi kiri kwamba matukio yale yalimfanya akachukia watu wa kabila lake la Kikuyu na hakuwa anataka kuoa Mkikuyu kabisa lakini mipango ya Mungu ilivyo tofauti, bado akampa Mkikuyu ambaye aliibukia kumpenda sana na miaka kumi na minne baadae, ndoa iko imara kama daima, ila si mtaa wa Embakaksi Nairobi.

Miaka miwili iliyopita Mwangi na familia yake kwa maana ya mkewe na wanao wawili walifanya filamu kuhusu matukio ya kutoka chaguzi za 2007, 2013 nqa 2013, filamu ambayo inakwenda kwa jina la 'Softie' ambayo inaelezea uhalisia wqa mambo nyakati za chaguzi kuu nchini. ni filamu ambayo imefanya vizuri kabisa katika kumbi za sinema ndani na nje ya Kenya.

Kwa wale mnaopuuza kauli kwamba mapenzi ni kama magugu yanayochipuka sehemu yoyote, basi kaifuatilie hadithi ya mapenzi ya Mwangi na mkewe yalivyoanzia, huenda hilo litawasaidia kubadili fikira, bure hivo useja na ukapera vitawaganda ja kupe na ngozi.