Nyota wa Bongo Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha uhusiano mzuri kati yake na watoto wake na Zari Hassan.
Licha ya kuwa na jumla ya watoto wanne wanaojulikana, mara nyingi Diamond ameonekana kuwapendelea zaidi watoto wawili ambao alipata na mwanasoshaiti huyo kutoka Uganda.
Jumanne wakati dunia yote iliadhimisha siku ya wanawake duniani staa huyo wa Bongo alitumia fursa hiyo kusherehekea mamake Sanura Kassim almaarufu Mama Dangote, dadake Esma Platnumz, bintiye Tiffah Dangote na msanii wake Zuchu.
Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Diamond alipakia picha za wanne hao na kuziambatanisha na emoji za upendo.
Baba huyo wa watoto wanne aliambatisha picha ya bintiye na ujumbe, "Maneno hayawezi kueleza upendo wangu kwako Tiffah Dangote."
Diamond hakusherehekea baby mama wake yeyote ama mpenzi wake wa zamani yeyote katika siku hiyo maalum kwa wanawake.
Licha yake kumsherehekea Zuchu, mapema mwaka huu Diamond alipuuzilia mahusiano ya kimapenzi naye huku akidai kuwa yuko kwenye mahusiano na mwanadada mwingine asiye maarufu.