Mahaba ya Diamond Platnumz na Zuchu jukwaani yafufua tetesi za mahusiano yao

Muhtasari

•Wababe hao wa muziki walipokuwa wanatumbuiza walionekana wakikumbatiana mara kwa mara na kutazamana kwa macho ya mahaba.

•Mashabiki wao wengi wamesifia muunganisho mzuri kati yao wakati wa matumbuizo hayo huku wengine wakidai wanaonekana vizuri pamoja.

Diamond na ZXuchu wakati wa uzinduzi wa EP ya FOA
Diamond na ZXuchu wakati wa uzinduzi wa EP ya FOA
Image: HISANI

Kanda ya video ambayo inaonyesha mastaa wawili wa Bongo, Diamond na Zuchu wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa FOA The EP imekuwa ikienezwa sana mitandaoni katika siku za hivi majuzi.

Wasanii  hao wawili ambao kwa kipindi kirefu sasa wamedhaniwa kuwa wapenzi walicheza wimbo 'Mtasubiri' pamoja katika hafla hiyo.

Ingawa wawili hao walipuuzilia mbali madai ya kuwa kwenye mahusiano,mdahalo mkubwa umechimbuka  kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kutokana na  jinsi  walivyotumbuiza.

Wababe hao wa muziki walipokuwa wanatumbuiza walionekana wakikumbatiana mara kwa mara na kutazamana kwa macho ya mahaba.

Wimbo 'Mtasuburi' ambao wawili hao walicheza ni wa mapenzi na ulisikika kama ujumbe kwa mahasidi wa penzi lao. 

Mashabiki wao wengi wamesifia muunganisho mzuri kati yao wakati wa matumbuizo hayo huku wengine wakidai wanaonekana vizuri pamoja.

Hizi hapa hisia za mashabiki baada ya kutazama video hiyo:-

Mariam Issa: Nimetabasamu muda wote...🔥🔥🔥🔥 kemia yao, sauti, utendakazi 🔥

Gogift: Hawaonekani kuwa wanaimba tu bali wanaelezana mioyo yao.

Keki Plus: MashaAllah MashaAllah hawa watu wanafanya watu waone mapenzi matamutamu...zuhura anakwambia ni kweli ila inawahusu nini🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣komesha kiranga🤣🤣🤣

Souvenir Weber: Hii couple naipenda sana sinaga uteam ila Diamond na Zuchu wanafaa kuwa wenza na kufanyakazi pamoja. Nimetizama hii nyimbo zaidi ya 10 times haichoshi.

God's daughter: Hawa wawili wana haki wana muunganisho mzuri wa mapenzi.. Diamond alihitaji msichana mnyenyekevu kama zuchu banaa,hao wengine wanamke wa mjini,ma slay Queen🙊kuvumiliana na Diamond Itakua ngumu..wanakaa vizuri pamoja.

Mwezi jana uvumi wa mahusiano ya Zuchu na Diamond ulivuma sana kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Wawili hao walijitokeza kupuuzilia mbali uvumi huo na kudai kuwa tayari kila mmoja wao ako kwenye mahusiano mengine.