King Kaka azungumzia kutopromote album ya Arrow Bwoy

Muhtasari

• Alisema kwamba amekuwa akisafiri, hivyo kukosa muda wa kuisikiliza album hiyo.

• King Kaka aliweka wazi kwamba hakuna tofauti zozote kati yake na Arrow Bwoy.

Image: INSTAGRAM// KING KAKA

Rapa matata kutoka humu nchini, King Kaka hatimaye amefunguka kuhusu kitendo chake cha kutopost na kusambaza album ya Arrow Bwoy.

Akizungumza katika mahohiano na mwanablogu 2mbili, King Kaka alisema kwamba hakuna ugomvi wowote na msanii huyo na kukiri kwamba anamtakia kila la kheri katika safari yake ya muziki.

King Kaka alisema kwamba amekuwa na safari za mara kwa mara katika mataifa ya ughaibuni kwa hivyo hajapata muda kuisikiliza album hiyo na kuahidi kwamba atatenga muda na kuzichambua nyimbo kwenye album ya Arrow Bwoy.

"Nimekuwa na safari za hapa na pale lakini nikitulia nitasikiliza album yake," King alisema.

Mwanamuziki huyo alidokeza kwamba Arrow ni msanii anayejituma katika kazi zake na kwamba atazidi kufanikiwa katika chochote anachokifanya.

Ifahamike kwamba kipindi cha nyuma Arrow Bwoy  alikuwa amesajiliwa chini ya lebo ya Kaka Empire inayomilikiwa na King Kaka.

Pia aliwataka mashabiki kumpa sapoti Arrow Bwoy na kununua muziki wake kuutoka kwa album ya #Focus.

Kulingana na Arrow, alihisi kwamba ulikuwa wakati mwafaka wa kutanua mbawa zake na kujisimamia mwenyewe katika kazi zake za muziki.