"Sina nguvu, sina pesa!" Onyi wa Real Househelps of Kawangware aomba msaada

Muhtasari

•Amedai kwamba mikakati mikali ya kudhibiti maambukizi ya Corona amabyo iliwekwa miaka miwili iliyopita ilimpokonya kazi zake za kuigiza na kutumbuiza katika hafla mbalimbali.

•Alifichua kuwa ana wake watatu ambao wamemzalia watoto watano ila hakujakuwa na uhusiano mwema nao kutokana na hali yake.

Mwigizaji Onyi
Mwigizaji Onyi
Image: HISANI/ TRHK YOUTUBE

Mwigizaji wa zamani wa kipindi cha Real Househelps of Kawangware, Onyi, amefilisika na kwa sasa hana makazi.

Onyi ambaye pia ni mwanamuziki na mchekeshaji amesema kuwa janga la Corona lilimuathiri vibaya na kuchangia sana katika hali yake mpya ya kusikitisha.

Amedai kwamba mikakati mikali ya kudhibiti maambukizi ya Corona amabyo iliwekwa miaka miwili iliyopita ilimpokonya kazi zake za kuigiza na kutumbuiza katika hafla mbalimbali.

"Hapo mbeeleni kila wikendi ningekuwa natumbuiza katika harusi fulani, sherehe za kuadhimisha siku ya kuzali na hafla zingine zote. Lakini hawakutaka watu washikane. Watu walitakiwa kukaa mbali na mwingine, kuvaa barakoa na mengine. Haingeweza kufanya kazi. Hakuna kazi tulikuwa tunapata," Onyi alisema akiwa katika mahojiano na Mzuka Kibao TV.

Alisema kazi zilipokosekana alilazimika kuhama kutoka nyumba ya kupanga na kuenda kuishi kwa nyumba zinazomilikiwa na dadake kwa kuwa hangeweza kumudu kodi.

"Nishawahi fungiwa nyumba. Hata siendi kuigiza siku hizi. Nataka  kazi. Nipewe kazi," Onyi alisema.

Mwigizaji huyo alieleza kuwa kwa sasa amekuwa akikaa nyumbani na kuzunguka tu mitaani kwa kuwa hana kazi ya kafanya. Alikiri kwamba amekuwa akibugia vileo ili kuweza kupata usingizi kwani haijakuwa rahisi kwake.

Pia alifichua kuwa ana wake watatu ambao wamemzalia watoto watano ila hakujakuwa na uhusiano mwema nao kutokana na hali yake.

"Mimi sina nguvu. Sina pesa ata kidogo. Ata mke wangu tunakosana naye kwa sababu ya hayo tu. Niko na watoto watano. Wawili nimezaa na mke wangu ambaye yuko Sweden, wengine wawili nimepata na mke wangu ambaye yuko Kisii, mwingine mmoja yuko Marekani. Hatusikizani kabisa kwa kuwa sina kazi. Mwanaume ni pesa," Alisema.

Onyi amesema anajuta sana kutowekeza wakati alikuwa na pesa. Alikiri kwamba alikuwa na mazoea ya kutumia pesa bila mpango.

Amewasihi wanasiasa kujitolea kusaidia wasanii huku akidai kuwa wengi wao wanaumia katika ukimya. Pia amewaomba wa