Mwijaku asema yeye ndiye mshauri wa Diamond Platnumz

Muhtasari

• Mwanahabari Mwijaku amesema kwamba yeye ndiye mshauri mkuu wa Diamond Platnumz.

• Amesema kwamba anachukia sana Simba anapokosa kufuata ushauri wake.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Mwijaku

Mtangazaji na mfanyibiashara kutoka Tanzania, Mwijaku sasa anasema kwamba yeye ndiye mshauri mkubwa wa Diamond Platnumz.

Mwijaku amesema kwamba baadhi ya maamuzi makubwa na ya maana anayoyafanya Simba, anapata ushauri kutoka kwake.

Aliongezea kwamba kuna mambo mengi wamezungumza ila Diamond hawezi kuyaweka hadharani.

"...Hawezi kuonyesha mawasiliano yangu mimi na yeye kwa mtu yeyote,mshauri wake mkubwa ni mimi. Si mmemsikia kwenye chombo chake cha habari kaongea," alisema Mwijaku.

Alikiri kwamba ameonekana kuwa mkali na kumsuta Simba kwa sababu anafanya maamuzi ndivyo sivyo.

Mtangazaji huyo alisema kwamba yeye ni miongoni mwa Watanzania wachache ambao wana kisomo kikubwa na hivyo hafai kuchukuliwa poa tu.

Aidha alisema kwamba Diamond Platnumz hayupo kwenye orodha ya wanamuziki kumi  bora Afrika.

Ifahamike kwamba kwa kipindi kirefu sasa, Mwijaku ameonekana kuegemea upande wa Alikiba na Harmonize akisema kwamba ndo wanaoelewa muziki na gemu la burudani kwa ujumla.