Usipofungua kioo watasema unaringa! Ankoo Zumoo amsuta shabiki aliyeiba miwani ya Irene Uwoya

Muhtasari

• Ankoo Zumo ameonekana kukasirishwa na kitendo cha shabiki kuiba miwani ya mwanafilamu Irene Uwoya.

• Alisema kwamba mashabiki wanapaswa kutoa mazingira mazuri kwa wasanii wanapotangamana nao.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Ankoo Zumo

Mwanafilamu kutoka Tanzania, Ankoo Zumo amemtupia vijembe shabiki ambaye alionekana akiiba miwani ya Irene Uwoya.

Kupitia aliyoipakia katika mtandao wake wa Instagram, shabiki huyo anaonekana akinyakua kwa nguvu miwani aliyokuwa ameivalia Uwoya.

Inasemekana Uwoya alikuwa katika harakati za kutangamana na mashabiki wake wakati kitendo hicho kilipotokea.

Kulingana na Zumo, hulka kama hizo ndizo zinazowafanya mastaa wengi kutotangamana kwa urais na mashabiki wao.

"Usipofungua kioo watasema unaringa, haya sasa kama hiyo miwani ilikuwa kwa ajili ya matatizo ya macho utamuuzia nani?" Zumo aliandika.

Baadhi ya mashabiki na wasanii walionekana kushangazwa na tukio hilo huku wakiwarai mashabiki kukoma hulka hizo.

Japo Uwoya hajazungumzia tukio hilo mpaka sasa, alionekana kukasirishwa nalo.