logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Drake, msanii bora wa mwaka kitengo cha Hiphop

Drake aliwapiku wasanii nguli kama Lil Baby, Megan Thee Stallion, Pop Smoke na Moneybagg Yo.

image
na Davis Ojiambo

Burudani23 March 2022 - 05:38

Muhtasari


  • • Drake azidi kutamba kwenye hiphop baada ya kushindqa tuzo kwenye hafla ya I Heart Radio Music Awards jijini Los Angeles.
Drake

Tamasha ya kutoa tuzo za mwaka huu za I Heart Radio Music Awards ilifanyika usiku wa Jumanne katika ukumbi wa Shrine Auditorium jijini Los Angeles nchini Marekani ambapo wasanii mbalimbali walijinyakulia tuzo katika vitengo tofauti tofauti.

Tukio kubwa zaidi ni lile la msanii nguli wa hiphop, Drake kushinda tuzo ya msanii bora wa mwaka wa 2022 katika kitengo cha hiphop kwa kuwabwaga Lil Baby, Megan Thee Stallion, Moneybagg Yo na Pop Smoke.

Katika kitengo cha msanii wa kiume bora wa mwaka, Lil Nas X alibeba siku mabegani kwa kuibuka mshindi mbele ya mastaa wengine kama Ed Sheeran, Drake na Justin Bieber waliokuwa wakimenyana katika kitengo hicho.

Bara la Afrika pia lilipata uwakilishwaji japo finyu ambapo collabo ya Wizkid na Tems ilishinda katika kitengo cha ngoma bora ya Hiphop ya mwaka.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved