Wakfu wa Kush Tracey watoa nepi kwa zaidi ya kina mama 300 Pumwani

Muhtasari

• Msanii na mtangazaji Kush Tracey alitembelea hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani na kusambaza nepi kwa kina mama zaidi ya 300.

Msanii Kushy Tracey
Msanii Kushy Tracey
Image: Instagram

Msanii wa injili na mtangazaji Kush Tracey aliwasha taa za kuhanikiza furaha nyusoni mwa kina mama zaidi ya 300 katika hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani jijini Nairobi baada ya kuwazawidi diaper za watoto katika wadi za hiyo taasisi.

Kush Tracey alifanya ziara ya kushtukisha katika hospitali hiyo na kina mama waliokuwa wamejifungua na wamo kwenye wadi walipokezwa vifaa hivyo vya malezi ya watoto wachanga, jambo ambalo hawakuwa wamelitarajia.

Kush Tracey aliandika kwenye Instagram yake na kusema kwamba vifaa hivyo vilifadhiliwa na kampuni ya Huggies Diapers na kusambazwa katika hospitali hiyo na wakfu wake wa Kush Initiative ambao alianzisha ili kueneza upendo wa Yesu, fadhila na huruma kwa wale wanaomtafuta awezaye kuokoa na kubadilisha hali za maisha.

“Leo tumetembelea hospitali kubwa ya uzazi barani Afrika na ya 2 duniani. Hospitali ya kujifungua kina mama ya Pumwani na kupata fursa ya kusambaza diapers za Huggies #HuggiesDiapersDrive kwa wodi na akina mama mbalimbali ndani ya taasisi hiyo. tumetangamana na wanawake zaidi ya 300 katika wadi 6 tulizoweza kutembelea,” aliandika Tacey.

Msanii huyo alianza muziki kama msanii wa ngoma za dunia kabla ya kuokoka na kuanza kusambaza injili ambapo pia alipata ufunuo wa kuanzisha wakfu huo wa kuwasaidia watu wenye mapungufu mbalimbali na kuwaleta karibu na Mungu.