Mtangazaji na mfanyibiashara mashuhuri Betty Kyallo ameweka wazi kwamba kwa sasa hachumbiani na mwanaume yeyote.
Betty ambaye alitimiza miaka 33 hivi majuzi hata hivyo amesema kwamba anafurahia hali yake mpya.
"Nilisema nipo single na nina raha. Mara kwa mara walakini wanaume hunichanganya kidogo kidogo na kunitumia maua, chokoleti na Champagne," Betty alisema kwenye mahojiano ya hivi majuzi na Citizen Digital.
Mama huyo wa mtoto mmoja alieleza kwamba bado anamsaka mwanaume atakayestahiki kuwa baba mzuri kwa bintiye Ivanna na kwa watoto wengine atakaopata naye.
Alifichua kwamba anakusudia kupata mtoto mwingine mmoja wakati atakapopata mwanaume atakayekidhi matakwa yake kwa mume.
"Ivanna amekuwa akinishinikiza kuwa anataka mtoto. Amekuwa akanisukuma miaka mitatu ambayo imepita. Bado nasaka baba anayestahili kwa Ivanna na mtoto atakayekuja. Hadi wakati huo, sipangi kupata mtoto nimlee pekee yangu tena," Alisema.
Betty alifichua kwamba kuna ushirikiano mzuri katika malezi ya bintiye kati yake na aliyekuwa mumewe, Dennis Okari