'Lazima nikate maji ili nipate usingizi,' Onyi akiri kuzama ulevini, aomba Wakenya wakome kumkejeli

Muhtasari

•Baba huyo wa watoto watano alifichua kwamba huwa analazimika kupiga maji kila siku ili aweze kupata usingizi.

•Amewaomba Wakenya kukoma kukejeli hali yake huku akifichua kwamba matendo yao yamemwathiri sana binti yake aliye katika kidato cha tatu.

Mwigizaji William Okore almaarufu Onyi
Mwigizaji William Okore almaarufu Onyi
Image: SCREEN GRAB// TUKO EXTRA

Mwigizaji William Okore almaarufu 'Onyi' kutokana na kipindi cha Real Househelps of Kawangware amekiri kwamba masaibu yaliyomkumba baada ya janga la Corona kusimamisha kazi zake za usanii yamemwathiri sana kisaikolojia.

Akiwa kwenye mahojiano na Tuko Extra, Onyi alifichua kwamba huwa analazimika kupiga maji kila siku ili aweze kupata usingizi.

Baba huyo wa watoto watano amelalamika kwamba amekuwa akikejeliwa sana mitaani tangu alipofilisika.

"Mimi hukunywa, nisteam ili nipate usingizi kwa sababu sifikirii. Sina nafasi na wakati wa kufikiria. Nikikutana na mtu kwa njia, ananitoanisha eti sina kitu. Ata ombaomba nikikutana naye mjini ananiuliza kwani kazi kuliendaje.. wacha nikate maji kidogo ili nipate usingizi kwa sababu nikiingia kwa nyumba, mtu amenitukana vibaya nami nimeichukulia tu kwa roho," Onyi alisimulia.

Mwigizaji huyo alisema Wakenya hawajaupokea wito wake wa msaada vizuri. Alisema kwamba amekuwa akikejeliwa na kutusiwa sana mitandaoni.

Amewaomba Wakenya kukoma kukejeli hali yake huku akifichua kwamba matendo yao yamemwathiri sana binti yake aliye katika kidato cha tatu.

"Binti yangu yuko active kwenye mtandao. Imemwathiri. Anashindwa ikawa vipi watu wanamwambia babake vile," Alisema.

Amesema kwamba anajuta kujitokeza na kusimulia masaibu yake kutokana na mapokezi mabaya ambayo amekutana nayo.

Onyi ametoa ombi kwa Wasamaria wema kumsaidia kwa kazi. Amesema yupo tayari kufanya kazi ya yoyote inayohusu sana