Hakuna mwanamke mzuri kama Hamisa Mobetto, Mwijaku ampa makavu Zuchu

Muhtasari

• Mwijaku amesema kwamba hakuna mwanamke mrembo zaidi ya Hamisa Mobetto huko Tanzania.

• Amemtaka Zuchu kutojigamba sana kwa kuwa karibu na Diamond Platnumz.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Hamisa Mobetto

Mwanahabari kutoka Tanzania, Mwijaku amempa makavu Zuchu kwa kile anachokisema kwamba anavimba kutokana na ukaribu wake na Diamond Platnumz.

Akizungumza na mwanablogu mmoja, Mwijaku alimtaka Zuchu kufahamu  kwamba kulikuwa na wanawake warembo zaidi katika maisha ya Simba ila hawapo naye kwa sasa.

Mwijaku alimshauri Zuchu kumlazimisha Diamond Platnumz amuoe badala ya kuchezena.

Kauli hii ya Mwijaku ilijiri wakati ambapo pia  Khadija Kopa ambaye ni mamake Zuchu alitoa kauli tata akisema kwamba yeye ndiye amezaa mtoto ila wazazi wengine ashakum si matusi wamekunya.

Aidha, amesema kwamba Zuchu amefanya vizuri kimuziki ila bado ni mchanga kiakili na anapaswa kufanya maamuzi ya busara katika maisha yake.

Japo Zuchu na Diamond hawajaweka wazi  kwamba wanachumbiana, kuna ishara nyingi za wazi ambazo zinaonyesha pengine kuna kitu kinaendelea kati yao.