logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mnaiga sana, tuonyeshe logbook. Notiflow amlipua Erick Omondi

Notiflow amesema kwamba kuna wasanii wanaiga mambo ili kufurahisha mashabiki.

image
na

Habari01 April 2022 - 06:07

Muhtasari


Notiflow amesema kwamba tangu amzawidi mpenziwe watu maarufu wamekuwa wakiiga sana alichokifanya.

Amemtaka Erick Omondi kuonyeshana 'logbook' ya gari alilomnuulia mpenzi wake.

Instagram, KWA HISANI

Msanii Notiflow amemtupia makavu Erick Omondi baada ya mcheshi huyo kumnunulia gari mpenzi wake.

Notiflow kupitia ujumbe aliochapisha katika insta story yake, alisema kwamba mastaa wengi wanaiga kitendo chake cha kumzawidi mpenziwe gari ili kuwafurahisha mashabiki ila yote ni uongo.

Aliwataka wasanii kuishi kulingana na uwezo wao wala sio kufanya vitu ili kuufurahisha umma na kuwapiga vita wasanii wenzao ambao wanafanya mambo makubwa.

Kichuna huyo alimtaka Erick Omondi kuweka wazi risiti za gari alilomnunulia mpenzi wake [Lynne] , kwa sababu anahisi kwamba kilikuwa kitendo cha kutafuta kiki tu.

Kwa upande wake Erick Omondi alimtaka Notiflow kukoma kumtaja kwa kuwa hawapo kwenye viwango sawa.

"Ambieni huyo chokora asiwai ita jina yangu tena," Omondi aliandika.

Notiflow alipakia logbook ya gari alilolinunua katika mtandao wa Instagram, kuonyesha uhalisia wa kitendo chake.

Je unaamini wasanii wanaonyesha maisha tofauti mitandaoni ili kuwafurahisha mashabiki?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved