Sifanyi show, hawawezi kunilipa - Hamisa Mobetto

Muhtasari

• Hamisa Mobetto amesema kitendo cha mapromota kumchukulia poa kimemsabbabishia yeye kukosa kufanya show.

• Amesema kwamba maamuzi hayo yanalenga kuepusha mvutano kati yake na washikadau wa burudani.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Hamisa Mobetto

Msanii na mfanyibiashara kutoka Tanzania Hamisa Mobetto ameweka wazi sababu zake za kutofanya shows.

Mobetto amesema kwamba mapromota wengi wanawachukulia poa wasanii na kuwalipa kiasi kidogo cha hela.

Kulingana naye, mapromota wengi wanawadhulumu wasanii baada ya kufanya show wakidai kwamba wanaitisha kiasi kikubwa cha pesa ambacho

"Kwahiyo unaombaje msanii aje kufanya shoo, halafu baada ya kazi unadai ni ghali sana na kumfukuza eti unaweza kupata msanii mwengine," Mobetto aliandika.

Msanii huyo amekashifu washikadau wanaowakosea heshima wanamuziki akisema kwamba hiyo ni ajira kama nyingine.

Hamisa alikiri kwamba anafanya muziki kujifurahisha tu kwa sababu hataki kugombana na mapromota wa nchini humo ambao pia hawawezi kumudu bei yake ya kupanda jukwaani.

Ifahamike kwamba Hamisa Mobetto ni moja kati ya wasanii wa kike ambao wanazidi kufanya vizuri ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.