Shindwe!Erick Omondi amzima shabiki aliyemtaka kuacha ucheshi

Muhtasari

• Erick Omondi amesema kwamba ataendelea na kazi yake ya ucheshi.

• Mashabiki pia walimsapoti wakisema kwamba amefanya kazi kubwa kuikuza sekta hiyo.

Mcheshi maarufu nchini, Erick Omondi amemzima vikali shabiki ambaye alimtaka aache kazi yake ya ucheshi na.

Shabiki huyo alimtaka Omondi kuzingatia katika kuanzisha familia na kulea watoto.

"Erick sasa unapaswa kustaafu uanzishe familia," shabiki huyo aliandika.

Kauli hiyo ilijiri baada ya Omondi kupakia video kwenye mtandao wake wa Instagram, akiwa jukwaani na Churchill huko Nakuru.

Omondi alionyesha kukasirishwa kwake na kauli hizo huku akishikilia kwamba atazidi kusalia kwenye gemu hilo kwani hiyo ni talanta yake.

"Riswaaa, shindwe shetani mweusi, mchawi," Omondi alimjibu shabiki huyo.

Baadhi ya mashabiki walikubaliana kwamba mcheshi huyo anapaswa kuwaachia chipukizi wengine nafasi, huku asilimia nyingine ya mashabiki wakionekana kumtaka Omondi kuendelea na kazi anayoifanya kuikuza sekta ya ucheshi nchini.

Ifahamike kwamba rais huyo wa wacheshi Afrika amekuwa mstari wa mbele kupigania haki za wasanii hata kukamatwa na polisi.