Rotimi afurahisha wanamitandao kwa kumfunza mwanawe jinsi ya kuomba

Muhtasari

• “Tangulia na ungoza kama mfano. Waanzishe mapema na kumjua Mungu na pia jinsi ya kuwa na maongezi na Mungu,” aliandika Rotimi kwenye Instagram yake.

Rotimi na mwanwe wakiwa katika sala
Rotimi na mwanwe wakiwa katika sala
Image: Instagram

Mpenzi wa aliyekuwa mtangazaji na mwanamuziki wa Tanzania Vanessa Mdee, Rotimi kutokea Marekani ameteka mtandao wa Instagram baada ya kupakia picha akiwa na mwanawe ambapo anamfunza jinsi ya kupiga sala na kuomba Mungu.

Mwanamuziki Rotimi ambaye alimuoa Vanessa Mdee baada ya mwanamama huyo kutengana na aliyekuwa mpenzi wake mwanamitindo na msanii Juma Jux alipakia picha hiyo na kuifuatisha kwa maneno kwamba ni vizuri kuwafunza watoto masuala ya uchamungu wangali bado wadogo.

“Tangulia na ungoza kama mfano. Waanzishe mapema na kumjua Mungu na pia jinsi ya kuwa na maongezi na Mungu,” aliandika Rotimi kwenye Instagram yake.

Mashabiki wengi waliotoa maoni yao kwenye post hiyo wamemmiminia sifa kochokocho msanii huyo kwa kuonesha picha nzuri ya kumfunza mtoto mdogo njia za Mungu hata kabla ya kutinga mwaka mmoja.

Katika mahojiano fulani mwezi mmoja uliopita, Rotimi alifunguka jinsi anavyojisikia kuwa baba na mazingira yalivyo katika shughuli nzima ya ulezi wa mwanawe.

Kwangu huo ni wakati wa kupumua na kuwa na familia yangu na kuangazia mambo yangu mazuri ambayo najali zaidi. Borake ananiona na kuona jinsi tulivyo na kusoma kadri iwezekanavyo, huo ni wakati muhimu zaidi kwangu. Ni vizuri kuona akikua kila siku” Rotimi alisema katika mahojiano kuhusu ulezi wa mwanawe.