Kama sio pasaka ningekuwa nishaakununulia chopa-Sandra Dacha amsherehekea Akothee

Muhtasari
  • Marafiki, mashabiki na familiawalimtumia msanii huyo jumbe na kumtakia heri njema siku yake ya kuzaliwa
Akothee
Image: Facebook

Wikendi iliyopita majasirimali na msanii maarufu nchini Akothee alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kuadhimisha miaka 41.

Marafiki, mashabiki na familiawalimtumia msanii huyo jumbe na kumtakia heri njema siku yake ya kuzaliwa.

Binti wa kwanza wa mwanamuziki huyo, Vesha Okello alibainisha kwamba mzazi huyo wake  ametekeleza jukumu lake la mama ifaavyo.

"Yeye ni mjasiri, mbunifu, mwenye upendo, anayefanya kazi kwa bidii. Lakini zawadi yake kubwa ni kuwa mama.  Kheri za siku ya kuzaliwa kipenzi changu. Wewe ni nyota inayong'aa. Hadi ukiwa na miaka 41  bado wewe ni mzuri. Unazeeka kama mvinyo mzuri," Vesha alimwandikia mamake.

Rue Baby kwa upande wake alimtaja mamake kama mtu jasiri zaidi aliwahi kukutana naye maishani.

"Mwaka huu mpya kwako naomba upate upendo na baraka. Kheri za kuzaliwa mama. Nakupenda mama," Aliandika.

Fancy Makadia ambaye ni mtoto wa tatu wa msanii huyo amesema siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mama ndiyo muhimu sana kwenye kalenda yake.

"Kuna siku 365 kwa mwaka lakini siku yako ya kuzaliwa inang'aa zaidi kuliko zote. Kheri za siku ya kuzaliwa mama," Alisema.

Muigizaji Sandra Dacha kwa upande wake alimshereheka Akothee kwa ujumbe wa kipekee huku akikiri kwamba kuwa rafiki yake ni moja wapo wa heshima zake kuu.

"Tunaokoa BORA kwa mwisho !!!Mum si you know how much you mean to me 🙈 wewe kama sio pasaka ningekuwa nishakununulia chopper!

Unapofikisha miaka 41, ninataka kukujulisha kuwa kuwa rafiki yako ni mojawapo ya heshima zangu kuu. Wewe ni maalum sana kwangu. Ubarikiwe daima @akotheekenya," Aliandika Dacha.