Mange Kimambi afichua ukweli wa Range Rover alilonunuliwa Kajala na Harmonize, "Aliazima!"

Muhtasari

• Mangi Kimambi ameufichua ukweli wote kuhusu gari aina ya Range Rover Harmonize alilomnunulia Kajala.

Image: HISANI

Wiki iliyopita msanii Harmonize alifanya kufuru ya karne baada ya kupakia gari kwenye mitandao yake ya kijamii likionesha jina la aliyekuwa mpenzi wake muigizaji kajala masanja kwenye nambari za usajiri ambapo alidai kwamba ni zawadi amemnunulia Kajala kaam njia moja ya kumbembeleza amrudie.

Harmonize alieleza kwamba aliamua kumnunulia gari hilo aina ya Range Rover kwa sababu alikuwa anajua fika mapenzi ya Kajala kwa magari ya aina hiyo.

Sasa mwanaharakati wa mitandaoni ambaye hachelewi kuwaingilia wasanii wa Bongo, namzungumzia Mange Kimambi, alijibwaga kwenye suala hilo zima la zawadi ya Range Rover kwa Kajala na kutumbua ukweli wote huku akimsuta Harmonize kwa kudanganya.

Je, alidanganya nini?

Kulingana na Mange Kimambi, gari hilo Harmonize alilodai kumnunulia Kajal ani uongo mtupu ambapo alifichua ukweli kwamba gari lile halikununuliwa bali aliazima na kupakia jina la Kajala kwenye eneo ya namba za usajiri na kupiga picha kisha baadae kujishaua nalo mtandaoni kama zawadi kwa ya pasaka kwa Kajala.

Kimambi aliweka wazi kupitia App yake ya Mange Kimambi kwamba gari hilo lilikuwa la mke wa meneja wa Harmonize!

Kajala amekuwa mgumu kumrudia Harmonize ambaye amekuwa akifanya vimbwanga mitandaoni akimtaka Kajala kumrudia baada ya mahusiano yake na mwanadada Briana kutoka Australia kugonga mwamba kavu.