(VIDEO) "Rayvanny ana sauti nzuri" Zari Hassan amsifia

Muhtasari

• Zari Hassan aliisifia sauti nzuri ya Raayvanny huku akisema ana uwezso mkubwa wa kuimba ila hapati promotions za kutosha.

Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Zari

Mwanamama na mjasiriamali Zari Hassan anayekipiga South Africa akitokea Uganda ameisifia pakubwa sauti ya msanii Rayvanny na kusema kwamba kila anapoisikia anahisi vizuri.

Katika Video ambayo imesambazwa na mtumizi mmoja wa mtandao wa Instagram, Zari anasikika akimsifia pakubwa Rayvanny ambaqpo anasema ana sauti nzuri ya kumtoa nyoka pangoni na kutabiri kwamba hichi ndicho kitu kikubwa kabisa kijazo katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, pengine baada ya aliyekuwa mume wake Diamond Platnumz ambaye walifanikiwa kuwa na watoto wawili pamoja.

Zari anazidi kusema kwamba licha na kwamab Rayvanny ana sauti nzuri lakini anakosa kitu kimoja cha muhimu sana katika Sanaa – Promotion.

“Rayvanny ana sauti nzuri. Rayvanny anaweza imba. Kitu tu anakosa ni promotion. Sijui ni kwa nini hapati promotions za kutosha, ni mwanamuziki mzuri sana,” Zari anaonekana na kusikika akimsifia Rayvanny.

Sifa hizi zinakuja saa chache tu baada ya Rayvanny kufuta utambulisho kwenye bio yake uliokuwa unamhusisha na uongozi wa lebo ya Diamond Platnumz, WCB Wasafi ambapo wengi walihisi ni kama ishara moja ya kujiondoa pale.

Wiki chache zilizopita katika filamu ya matukio ya kihalisia ya Young Famous and African iliyooneshwa kwenye mtandao wa Netflix, mwanamama Zari alimzomea wazi msanii Diamond kwa kumuacha upweke bila kumtetea wakati watu walikuwa wanamtupia matusi, kupelekea mahusiano yao kukatika.