Abel Mutua aomba mkewe msamaha kwa kumuacha 'lonely' ndani ya Shincity

Muhtasari

Abel Mutua amelazimika kuomba mkewe  msamaha baada ya mashabiki kumlipua mtandaoni.

Hii ni baada ya video kusambaa kwenye mtandao wa Instagram, ikimuonyesha mkewe akipiga densi pekee yake.

Abel Mutua
Abel Mutua
Image: Instagram KWA HISANI

Mwanafilamu na muigizaji matata humu nchini Abel Mutua amelazimika kuomba msamaha kwa mkewe baada ya mashabiki kumlipua mtandaoni kwa kile walisema kuwa alimtelekeza mkewe walipokuwa wakihudhuria hafla ya Shincity.

Katika video iliyokuwa ikisambaa katika mtandao wa Instagram, Judy Nyawira ambaye ni mkewe Mutua alionekana akipiga densi akiwa pekee yake huku rafiki zao wa karibu Njugush na Celestine Ndinda wakionekana kujifurahisha kwa pamoja.

Nyawira alionekana akimuuliza Mutua sababu kuu iliyopelekea kumwacha 'lonely' wakati wa hafla hiyo.

"Uko na mashtaka, kwa nini uliniacha pekee yangu ?" 

Mutua alijitetea akisema kwamba hakukusudia kufanya jambo lolote ambalo lingeibua maswali mengi na video hiyo pengine ilichukuliwa wakati ambapo alikuwa ameondoka kujihusisha na mambo nmengine ama kuzungumza na rafiki zake wengine.

"...Aki wakurugenzi mko na utiaji hata siwezi toka nikaongea na msichana mwengine mshaanza kunipiga mawe ," Mutua alisema.

Alisema waliochukuan video hiyo pengine walikuwa na malengo yao binafsi ya kujaribu kuzua gumzo na kuzua vurugu.

Judy Nyawira baadaye alikubali kumsamehe Abel na kuendelea na maisha yao kama kawaida.

Haya yalikuwa yanajiri katika hafla ya Shincity ambapo mastaa mbalimbali walikuwa wamehudhuria ili kutoa sapoti kwa msanii Nyashinski.