Diamond - Rihanna atakuwa kwenye albamu yangu, hii ama ile ijayo

Muhtasari

• "Kwa Mambo Yanayoendelea Kwa Rihanna Sasa, Inaweza Ikafanya Akawepo Kwenye Album. Hii Au Ijayo,” - Diamond Platnumz

Rihanna, Diamond Platnumz
Rihanna, Diamond Platnumz
Image: Instagram

Nguli wa muziki wa kizazi kipya katika ukanda wa Afrika Mashariki Diamond Platnumz anasema ndoto yake kubwa ni kufanya collabo ya moto na msanii nguli kutoka Barbados, Rihanna.

Akizungumza katika mahojiano kupitia shirika la habari la BBC baada ya hafla ya kuizikiza miziki yake kwenye EP ya FOA, Diamond alisema analenga siku moja kabla hajaacha kufanya muziki awe amekipiga pamoja na Rihanna.

Msanii huyo aliwahakikishia mashabiki wake kote ulimwenguni kwamba tayari mazungumzo baina ya pande zote mbili yamefanyika kwa mafanikio makubwa na huenda akawepo kama si kwa albamu yake ya sasa basi kwenye albamu ijayo watamuona na kumsikia Rihanna akitema cheche kwenye spika pamoja na Diamond.

“Ningependa Kufanya Kazi Na Rihanna, nahisi itakuwa ni ngoma kali sana, Kama Sio Kwenye Album Hii Basi Album Yangu Inayofuata, Tumeshaongea Na Rihanna Na Timu Yake Na Kila Kitu Kipo Sawa, Kwa Mambo Yanayoendelea Kwa Rihanna Sasa, Inaweza Ikafanya Akawepo Kwenye Album. Hii Au Ijayo,” alisema Diamond kwa hakikisho kubwa kwa mashabiki wake.

Maneno haya ya Diamond yanawiana na maneno ambayo yalitamkwa na msalishaji wake wa muziki S2Kizzy ambaye alidokeza kwamba huenda akawa katika project moja na Rihanna na sasa wengi wanaamini huenda katika collabo hiyo, S2Kizzy ndiye atakuwa nyuma ya ujanja na mirindimo ya beats.

Kwa sasa Rihanna ni mjamzito ambapo hivi majuzi uvumi ulisambaa kwamba huenda wameachana na mpenzi wake msanii A$AP Rocky kwa kile kilisemekana kwamba ni mpenzi wake huyo kuchepuka na mwanadads anayemcvhagulia fasheni ya viatu Rihanna.

Ila madai haya yalipuuziliwa mbali muda mfupi baadae na rekodi lebo ya TMZ.