logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Harmonize amtolea Kajala kibao kama njia ya kuomba msamaha

Harmonize amtolea Kajala kibao kama njia ya kuomba msamaha.

image
na Radio Jambo

Habari21 April 2022 - 10:43

Muhtasari


• Harmonize alisema kwamba Kajala ndiye mke wa ndoto zake.

• Alishikilia kwamba anaamini Kajala atamsamehea na waendeleze mahusiano yao.

Staa wa muziki kutoka Bongo, Harmonize ameamua kumtolea Frida Kajala kibao kama namna moja ya kuomba msamaha.

Kupitia ujumbe mrefu aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Kondeboy alisema kwamba Kajala ndiye mwanamke wa ndoto zake na anaamini watarejeleana.

Alimtaka Kajala kutosikiliza mambo na maoni ya watu kwa kuwa mapenzi ni ya watu wawili, hivyo changamoto zinapozuka zinapaswa kusuluhishwa ndani kwa ndani.

Alimshukuru kwa kuweka siri zao hasahasa kipindi alituhumiwa kumtumia picha za uchi mtoto wa Kajala [Paula Kajala].

"...Ila kwa kuwa una hofu ya Mungu ulinihurumia na ukalia pekee yako ukamkabidhi Mungu na bila shaka ukaniombea nifanikiwe tena kwa kasi kubwa. Niseme tu chozi lako lingenitesa mno," Harmonize aliandika.

Akionyesha ufahamu wake kwamba Kajala anahitaji muda zaidi ili kufanya maamuzi hayo mazito, Harmo alisema kwamba wimbo huo ndo ulikuwa kishawishi cha mwisho kujaribu kuliokoa penzi lao.

"...Napitia kipindi kigumu sana, na hiki ndo kitu cha mwisho naweza kukufanyia. Usisahau sauti na kipaji ndo vimefanya naitwa Harmonize," Kondeboy aliandika.

Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, Harmonize amekuwa akijaribu kumuomba msamaha, ila Kajala hajatoa tamko lolote mpaka sasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved