'Siwezi muacha mwanamume kwa kunicheza,'Huddah Monroe afichua haya

Muhtasari
  • Akitumia hadithi zake za Insta, Bi Monroe aliweka wazi kuwa watu pekee ambao hapendi kuburudisha maishani mwake ni waongo
Huddah Monroe
Image: Facebook

Mwanasosholaiti wa Kenya na mjasirimali  Alhuda Njoroge almaarufu Huddah Monroe amekiri kwamba hataachana na mwanamume ambaye anachumbiana kwa sababu tu alidanganya.

Akitumia hadithi zake za Insta, Bi Monroe aliweka wazi kuwa watu pekee ambao hapendi kuburudisha maishani mwake ni waongo.

"Siwezi kamwe kumuacha mwanaume kwa kudanganya. Lakini ningekuwa mwepesi kuondoka ikiwa ni mwongo. Mimi sio mama yako. Sitakupiga. Sisi ni watu wazima. Ishike kwa asilimia 100, hasa wanaume weusi hudanganya bila sababu hata kidogo,” Alisema Huddah.

Aliendelea kutoa mfano wa mpenzi wake wa zamani ambaye aliwahi kuwa mwongo mashuhuri - akisema uwongo kila wakati.

“Mpenzi wangu wa zamani alikuwa akisema uongo mdogo ambao hata akiwa mgonjwa sikuamini. Lazima nimwone huko ER na gauni la hospitali ili niamini. Anaweza kufa anifahamishe nikafikiri anacheza, maana nahitaji ushahidi kaka,” Huddah alilalamika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Huddah Cosmetics ambaye haogopi kamwe kusema mawazo yake, aliwashutumu wanaume weusi kwa kuwakatisha tamaa sana katika mahusiano.

“Nimechumbiana na mataifa mengi sana na kuchumbiana na mtu mweusi ni sawa na kuingia mase. Ni kazi ngumu sana, unaweza kwenda kiakili kwa urahisi. Na sababu ni mama yao. Ninyi nyote wanawake wenye watoto wa kiume, fanyeni vyema kwa kizazi kijacho cha wanaume weusi,” alishauri.