Baraka tele!Msanii Evelyn Wanjiru abarikiwa na mtoto wa kiume

Muhtasari
  • Msanii Evelyn Wanjiru abarikiwa na mtoto wa kiume
Evelyn Wanjiru na mumewe
Evelyn Wanjiru na mumewe
Image: Instagram, KWA HISANI

Habari za ujauzito wa msanii wa nyimbo za injili Evelyn Wanjiru zilipokelewa vyema na mashabiki, huku wengi wakitumia fursa hiyo kumpongeza.

Msanii huyo alikuwa amesubiri kwa miaka Kumi, ili kupokea baraka zake.

Huku mumewe akipakia picha ya mkewe na mwanawe kwenye ukurasa wake wa instagram alimshukuru Mungu kwa kifungua mimba wake.

Pia wanandoa hao wawili walificua kwama walibarikiwa na mtoto wa kiume amabye anafahamika kama Mshindi tarehe 6 Aprili.

"Tarehe 6 Aprili 2022 Mungu alitupa zawadi ya mtoto wa kiume!! Huu ni ushuhuda mimi na mke wangu tumekuwa tukimngojea Mungu kwa miaka 10 iliyopita.

Karibu duniani mtoto Mshindi Akweyu Agundabweni,familia yako yote inakupenda sana! Tunafurahi kukuona ukikua na kuwa mtu mkuu ambaye Mungu alikukusudia uwe! Wewe ni ndoto iliyotimia, sala iliyojibiwa na zawadi kuu kutoka kwa Mungu!

@evelynwanjiru_a Namshukuru Mungu kwa ajili yako mke wangu, wewe ni mwanamke bora na zawadi ya kweli uliyopewa na Mungu! Nakupenda! Asante kwa kubeba mtoto Mshindi kwa miezi 9 na kumleta kwenye sayari hii! Nimefurahiya na niko tayari kumlea pamoja nawe!" Alisema mumewe Evelyn.

Kwa upande wa Evelyn alimshukuru Mumewe kwa kuwa naye wakati wote.