Flossin Mauwano afafanua maana ya maandishi yake katika barabara za Kenya

Muhtasari

•Mule alisema alichora graffiti za 'Flossin Mauwano' kama tahadhari kwa madereva kuhusu ajali za barabarani.

•Alifichua kuwa aliacha kuchora baada ya Mamlaka ya Kusimamia Barabara za Kenya kumshtaki mahakamani na akapigwa marufuku.

Stephen Mule almaarufu Flossin Mauwano
Stephen Mule almaarufu Flossin Mauwano
Image: HISANI

Msanii Stephen Mule almaarufu Flossin Mauwano ameweka wazi kuwa michoro ambayo amefanya katika barabara mbalimbali nchini haina maana ya kihalifu.

Akiwa kwenye mahojiano na Ala C, Mule alisema alichora graffiti zile kama tahadhari kwa madereva kuhusu ajali za barabarani.

"Natetea usalama barabarani. Watu hustarehe kwa barabara na ni mauwano. Ni kampeni ya usalama wa barabara. Ujumbe wangu ni kupigania usalama barabarani," Mule alisema.

"Jina Flossin Mauwano linamaanisha Blackspot. Hiyo graffiti inafungua dereva macho. Inamuonyesha dereva kuwa mahali pale anahitaji kuwa makini zaidi anapoendesha gari,"

Msanii huyo alisema hali ya wazazi wake kupoteza maisha yao katika ajali ya barabarani ilipatia  kampeni yake msukumo mkubwa.

"Mwaka wa 1997 baada ya uchaguzi kulitokea ghasia. Wazazi wangu walikuwa na nyumba za kupanga huko Kibera lakini tulikuwa tunaishi Lang'ata. Walikuwa wanatoka kwa ploti zetu wakikuja nyumbani. Vita vikaanza na katika zile harakati za kutoroka wakapata ajali," Alisimulia.

Mule alifichua kuwa alianza kuchora barabara akiwa mdogo bado baada ya kupata ufunuo kutoka kwa marehemu baba yake.

Alifichua kuwa alichora graffiti yake ya kwanza katika barabara ya Langata. Wakati huo alikuwa katika darasa la saba.

"Niliona mzimu wa baba yangu. Alikuja akanipatia chupa. Wakati huohuo gari moja likapata ajali. Niliokoa mama mmoja. Kutoka wakati huo nikaanza kuchora. Nilichora graffiti ya mwisho jijini Kampala, Uganda," Alisema.

Mule alifichua kuwa mbali na Kenya na Uganda amewahi kuchora graffitti Dubai. Pia  alipuuzilia mbali madai kuwa yeye ndoiye alichora graffitti ya 'Flossin Mauwano' iliyo katika barabara mpya ya Nairobi Express Way huku akiweka wazi kuwasema alichora yake ya mwisho mwaka wa 2011.

Msanii huyo alieleza kuwa aliacha kuchora baada ya Mamlaka ya Kusimamia Barabara za Kenya (KeNHA) kumshtaki mahakamani na akapigwa marufuku. Alipuuzilia mbali madai kuwa yeye ndiye ali

Hata hivyo alisema kampeni zake zilisaidia sana katika kupunguza ajali za barabarani katika eneo la Nairobi.