Sikuwa nimekasirika-Bahati atoa sababu ya kulia baada ya kupoteza uteuzi wa ubunge wa Jubilee

Muhtasari
  • Bahati atoa sababu ya kulia baada ya kupoteza uteuzi wa ubunge wa Jubilee
Kevin Bahati,akihutubia wanahabari siku ya JUmatatu Aprili/25/2022 katika hoteli ya Luke Nairobi
Image: WILFRED NYANGARESI

Mpema wiki hii msanii na mwaniaji wa ubunge wa Matjare Kevin Bahati aligonga vichwa vya habari baada ya kushindwa kushikilia machozi yake.

Hii ni baada ya uteuzi wake wa ubunge kwa tikii ya Jubilee kubatilishwa na chama hicho.

Akiwa kwenye mahojiano akizungumzia wakati huo ambao ulimfanya avume mitandaoni Bahati alisema kuwa hakuwa amekasirika bali alikuwa analilia watu wa Mathare.

Kulingana na Bahati, alikuwa akiwalilia watu wa Mathare, ambao anataka kuwawakilisha katika Bunge la Kitaifa.

“Sikuwa na hasira nilikuwa naeleza tu mahitaji ya wananchi wangu, bungeni nitakuwa nawakilisha wananchi, mbunge na mtekelezaji, kwa hiyo nilikuwa nawakilisha wananchi, nilichukua machungu yao na kuyapeleka kwenye vyombo vya habari. mkutano

"Jana mumenikimbiza mbio sana, kwani mtu hawezi lia tu? ," Bahati alisema.

Sasa, anasema ameamua kushikamana na Uhuru wala si naibu wake kwa sababu yeye ni kiongozi aliyetiwa mafuta na Mungu.

“Kila kiongozi amepakwa mafuta na Mungu, kwa sasa kiongozi aliyewekwa kwenye kiti ni Uhuru, amalize muda wake aondoke. ," alisema.