Kama una mimba ya Rayvany mimi inanihusu nini,'Fahyvanny amjibu kipusa aliyedai ana ujauzito wa Rayvanny

Muhtasari
  • Fahyvanny amjibu kipusa aliyedai kuwa na ujauzito wa Rayvanny
Fahyvanny
Image: HISANI

Fahyvanny amepata umaarufu wake kwenye tasnia ya burudani kama mwigizaji wa video.

Baadaye alipata umaarufu mkubwa kwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii wa Bongo Raymond Shaban Mwakusya almaarufu ​​Rayvanny.

Wawili haowalibarikiwa na  mtoto wa kiume anayeitwa Jayden ambaye kwa sasa ana umri wa miaka mitano. Hata hivyo ni wazazi wenza tangu walipoachana.

Fahyma kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram ameshughulikia suala la mwanamke anayedai kuwa na ujauzito wa aliyekuwa mumewe Rayvanny.

Kwenye chapisho Fahyma alikuwa na hasira sana kwamba unaweza kusoma hasira yake kutokana na maneno yake.

Alimwonya bibi huyo akimwambia aache kumjumuisha katika ujauzito wake na Rayvanny. Hii ni kwa sababu haimjali wala kumsumbua.

"Mimi huwa sipendi kugombana ila wewe dada @jessyntibi umenifika kooni 😏 kutwa kwenye Dm yangu kunichamba na kuongea maneno yasiyo na maana please niache ✋ sasa kama una mimba ya rayvany mimi inanihusu nini mxieew 😏 niache staki @jessyntibi @jessyntibi umezidi hebu nisaidieni kwenda kumchamba 🤣🤣🤣🤣," Aliandika Fahyvanny.