Alitembea kilomita 22 akiwa na ujauzito wa miezi 8- Mcheshi YY asimulia magumu aliyoyapitia mama yake

yy
yy

Mcheshi YY ni mmoja wa wacheshi ambao wanafahamika sana nchni, kutokana na ucheshi wake katika tasnia ya burudani.

Huku nchi ikiadhimisha siku ya akina mama dunia siku ya Jumapili, watu tofauti na watu mashuhuri walichukua fursa hiyo kuwasherehekea watoto  wazazi wao.

Pia kuna wale waliwalimbikizia sifa wazazi wao kwa kuwlea kwa njia ya kipekee na hata kujikakamua katika maisha yao kuhakikisha wana maisha bora ya kuishi walipokuwa watoto.

McheshI YY kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram alimsifia mama yake na kusimulia magumu aliyoyapitia alipokuwa na ujauzito wa mdogo wake.

Kulingana na YY mama yake alikuwa anataembea kilomita 22 akiw na ujauzito wa miezi nane ili kuhakikisha amempelekea ada ya shule.

"Kufunga siku ya akina mama ni mwanamke mmoja ambaye ninaheshimika kuwa naye….Nilipokuwa kidato cha 2 katika shule ya upili ya Agoro sare alitembea jumla ya KM 22 kuniletea hundi ya benki huku akiwa na ujauzito wa miezi 8…alitoka shuleni saa kumi na moja jioni na sikujua alifika. aje home😭…zamani sikuwahi kuona ukubwa wake hadi nikawa mtu mzima…

Simchukulii kirahisi Mama…Mshauri na mcheshi wa familia yetu…Yeye ndiye mcheshi kuliko sisi sote….Namshukuru Mungu kwa ajili yako… Nina deni daima❤️ Happy Mother's day Nyar Luanda," YY Aliandika.