(+VIDEO)Tazama jinsi Rashid alivyooshwa kwa pesa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Muhtasari
  • Mkewe Lulu Hassan alikuwa miongoni mwa marafiki ambao walimwekea sherehe huku wakimuosha kwa pesa

Huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa mwanahabari wa runinga ya Citizen Rashid Abdalla alipokea zawadi tofauti na hata kuoshwa kwa pesa na marafiki zake.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram akisherehekea siku yake ya kuzaliwa alimshukuru mama yake kwa kuwa naye na kumlea tangu utotoni na baada ya baba yake kuaga dunia.

"Alhamdullilahi it’s my birthday. Asante mamangu kwa kila jambo najua haijakuwa raisi wewe kunilea peke yako baada ya baba kufariki lakini ulijitahidi. Nakuombea Mungu akusamehe dhambi zako, Mola akujalie neema na baraka, Maulana akupe umri mrefu wenye afya njema na amali njema."

Mkewe Lulu Hassan alikuwa miongoni mwa marafiki ambao walimwekea sherehe huku wakimuosha kwa pesa.

Hii hapa video ya sherehe hiyo huku Rashid akioshwa kwa pesa;