Nitafurahi sana nikiwa na wapenzi 4-Mbosso

Muhtasari
  • Kama Mwislamu, mwimbaji anaruhusiwa kuoa wake wanne. Jumuiya za Kiislamu zinaruhusu hadi wake wanne

Mwimbaji wa Tanzania Mbosso amefunguka kuhusu jinsi angefurahi kuwa na wapenzi wanne.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliandika;

“Ukiwa na mpenzi mmoja anakupa furaha. Imagine ukiwa na wapenzi wanne hayo mafuraha yake," Aliandika Mbosso.

Si mara ya kwanza mwimbaji anazungumza kuhusu kuwa na wapenzi wengi. Mnamo 2020 alisema kuwa wake wanne hawatoshi, angependelea kuwa na wanawake 15 hadi 20.

Alisema hayo kwenye harusi ya Esma Platnumz;

"Wakati bachelors kama sisi wanaona tukio kama hili, inatupa msukumo wa kuoa. Nadhani pia nitapata wanawake warembo hapa, huwezi jua, naweza kupata mke hapa.”

"Kusema kweli, wake wanne hawatoshi, nikipata hata 20 au kumi au 15, nitakuwa mzuri. Lakini kwangu, wanawake wanne ni wachache sana.”

Kama Mwislamu, mwimbaji anaruhusiwa kuoa wake wanne. Jumuiya za Kiislamu zinaruhusu hadi wake wanne. Mbosso tayari ni baba wa watoto watatu kutoka kwa wanawake tofauti.