logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kambua awatia moyo akina mama ambao wamewapoteza watoto

Pia aliweka wazi jinsi  siku ya akina mama ilimaanisha  kwake mwaka huu.

image
na Radio Jambo

Habari13 May 2022 - 12:01

Muhtasari


  • Kambua awatia moyo akina mama ambao wamewapoteza watoto
Mwanamuziki Kambua

Msanii wa nyimbo za injili Kambua kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefunguka aliyoyapitia baada ya kumpoteza mtoto wake huku akiwatia moyo akina mama ambo wamepitia hali kama yake.

Pia aliweka wazi jinsi  siku ya akina mama ilimaanisha  kwake mwaka huu.

Mtangazaji huyo ni miongoni mwa wanawake wengi ambao wamehisi uchungu wa kumpoteza mtoto; na ameshiriki faraja yake na wanawake ambao wamepitia hali hiyo hiyo.

Mama huyo wa mtoto mmoja kupitia mtandao wake wa Instagram, ameeleza jinsi alivyoachwa hatarini na kutokwa na machozi baada ya kufiwa na mtoto wake mchanga.

"Nimekuwa nikifikiria kuhusu Siku ya Akina Mama na ilimaanisha nini kwangu mwaka huu.

Sikuwahi kutarajia maporomoko ya hisia zilizokuja nayo. Namaanisha, ninashukuru sana kwa safari ya kimiujiza ambayo nimekuwa nayo, lakini moyo wangu pia unafahamu kikamilifu matukio ambayo yamesababisha uharibifu na kuniacha kabisa. Ni tamu chungu; kuwa na mtoto mchanga mikononi mwako, na kuwa na mwingine mbinguni. Nililia. Machozi mengi, mengi. Nilihisi kidogo kama ninakosa hewa, lakini bado niko hai huku moyo wangu ukipiga kwa nguvu sana.”

Aliendelea na ujumbe wa kutia moyo;

"Kwa mwanamke yeyote ambaye amepata uzoefu wa bahati mbaya kujua jinsi inavyojisikia kupoteza- iwe kuharibika kwa mimba, kuzaliwa bado, kupoteza mtoto ...

Kwa mwanamke yeyote ambaye ametazama miaka inavyosonga, akiona akina mama wakisherehekewa huku akiwa bado amesimama na mikono mitupu na matandiko ya vumbi…

Kwa mwanamke yeyote ambaye ametamani zaidi ya mtoto mmoja na inaonekana haifanyiki…”

Kambua ni miongoni mwa watu mashuhuri wachache ambao wamejitokeza kuelezea uchungu wao wa kumpoteza mtoto wao mchanga.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved