Terence Creative afunguka kuhusu kupoteza mtoto na mkewe Milly Chebby

Muhtasari
  • Milly na Terence walifichua kuwa baada ya miaka mitano ya kuchumbiana waliamua kupata mtoto
Terence Creative na mkewe Milly Chebby
Terence Creative na mkewe Milly Chebby
Image: Terence Creative//Facebook

Mchekeshaji kutoka Kenya na mtayarishaji wa maudhui ya Mtandaoni Terence Macharia maarufu Terence Creative amefunguka kuhusu kumpoteza mtoto na mkewe Milly Chebby kabla ya kupata binti yao Milla Netai.

Katika mazunumzo na mashabiki wake kwenye Instagram, Terence alitaja kwamba kupoteza ni moja ya nyakati za mkazo zaidi maishani mwake.

Mchekeshaji huyo alifichua hayo wakati alipokuwa akimtia moyo shabiki ambaye pia alimfungukia kuhusu kumpoteza mtoto wao.

"Pole sana na ujitie moyo @Millychebby na mimi tulimpoteza mtoto wetu kabla ya Milla, ilinisumbua sana lakini kilichotufanya tuendelee ni maombi na mara tukaanza kutafuta ujauzito mwingine na utakuwa mzima," Terence creative alifichua.

Mnamo 2019, Milly Chebby pia alifunguka kuhusu kuharibika kwa mimba na kumpoteza mtoto wake katika wiki ya 13 ya ujauzito mwaka wa 2017.

Milly na Terence walifichua kuwa baada ya miaka mitano ya kuchumbiana waliamua kupata mtoto, lakini kwa bahati mbaya ujauzito huo haukufika hatua ya mwisho (delivery).

Milly alisema kuwa ujauzito ulikuwa wa kawaida hadi wiki ya tano.