Watoto wako wanaweza kukupeleka kaburini mapema-Ushauri wa Akothee kwa wazazi

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amesimulia jinsi wazazi hujitolea kwa ajili ya watoto wao
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Tunapozungumzia msanii na mjarimali Esther Akoth almaarufu Akothee sio mgeni katika majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Akothee anafahamika kwa semi zake na jinsi ya kuwakosoa wwanawe na wanamitandao ambao wamevuka mipaka.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram msanii huyo amesimulia jinsi wazazi hujitolea kwa ajili ya watoto wao ilhali watoto wao hawawezi.

Pia alisema kwamba watoto wanaweza kukupeleka kaburini mapema usipokuwwa makini kama mzazi.

"Ukweli angalia wazazi watoto wako hawatatoa dhabihu kama ulivyojitolea kwa ajili yao.. uchungu wake ni kwamba wanapokuwa kwenye uchafu, wanarudi kwako wakati wote na wakati wanashida,watoto wako wanaweza kukupeleka kwenye mazingira magumu au mapema kwenye kaburi..ni baraka kuwa mzazi pia inaweza kuwa maumivu moyoni endelea tu,"Akothee Alisema.