Msanii Ibraah afichua jina la albamu yake ya kwanza,awashukuru mashabiki wake

Muhtasari
  • Msanii Ibraah afichua jina la albamu yake ya kwanza,awashukuru mashabiki wake
Ibraah
Image: Instagram

Msanii kutoka Tanzania Ibarrah na mabye amesajiliwa katika lebo ya muziki ya msanii Harmonize kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amefichua jina la albamu yake.

Mnamo Jumanne Mei 24, 2022 Ibraah alifichua kwamba albamu yake ya kwanza itaitwa The King of New School. Alifichua wakati alipokuwa akizindua jalada la albamu.

“Hatimaye albamu yangu ya kwanza imekamilika! Tunakuletea 'Mfalme wa shule mpya' Asante Mungu 🙏🏼 Haikuwa rahisi (Haikuwa rahisi)! Shukrani kwa wote waliosababisha kukamilisha hili (Shukrani kwa kila mtu ambaye ameunga mkono mradi huu hadi kukamilika kwake)! Shukrani kwa usimamizi wangu Konde Gang. Ahsanteni mashabiki ambao siku zote mmekuwa namimi."

Bosi wa Ibraah Konde Boy pia alishiriki upya jalada la albamu hiyo- akisema kwamba anajivunia hatua zote muhimu ambazo msanii wake amefikia tangu kuanzishwa kwake katika tasnia ya muziki.

"Ninajivunia wewe kaka nenda ukabadilishe mchezo #thekingofnewschool 🤴 na nasubiri hii," Harmonize alisema.

Ibrahim Abdallah Nammpunga jina halisi alisajiliwa chini ya Konde Music Worldwide mnamo Aprili 2020 wakati Harmonize akipanua himaya yake.

Aliachia wimbo wake wa kwanza uliopewa jina la Nimekubali ambao uligeuka kuwa wimbo unaompa sifa stahiki katika tasnia ya muziki Tanzania.