'Msinipigie simu usiku mkiwa mshaalewa,'Msanii Lady Jaydee awaonya watu wenye tabia hii

Muhtasari
  • Usemi wa Lady Jaydee wa umri wa miaka 42 sasa unaonekana kukera watumizi wengi wa mitandao ya kijamii hususan Twitter
LADY JAYDEE
Image: KWA HISANI

Msanii kutoka Tanzania Lady JayDee kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa twitter amewaonya watu ambao wanatabia ya kumpigia simu usiku hasa wakati wamelewa.

KUlingana na msanii huyo watu hao hufanya hayo ili kijionyesha wako karibu naye, ilhali hawaungi mkono kazi yak.

"Watu mnaonifahamu msiwe mnanipigia simu usiku mkiwa mmeshalewa baada ya kusikia nyimbo zangu huko mlipo ili watu waone mna ukaribu na mimi wakati you don’t even support my businesses wala shows hamji. Kuweni outsiders tu siwa appreciate wala nini #FakeAss 😏," Msanii huyo Aliandika.

Usemi wa Lady Jaydee wa umri wa miaka 42 sasa unaonekana kukera watumizi wengi wa mitandao ya kijamii hususan Twitter.

Msanii huyo amekawia bila kuto kibao kipya, huku kibao cha mwisho akitoa akiwa amshirikiana na staa wa bongo Harmonize mwaka mmoja uliopita.