Sijawahi predict mshindi akaanguka-Ben Githae adai

Muhtasari
  • Ikumbukwe kwamba mwaka wa 2017 Ben Githae aliunga mkono chama cha kisiasa cha Jubilee kilichokuwa kinaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na naobu wake William Ruto
Image: INSTAGRAM// BEN GITHAE

Msanii wa nyimbo za injii Ben Githae kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook, amedai kwamba ahajawahi tabiri chochote na kukosa kutokea.

Msanii huyo amekuwa akiunga mkono muungano wa Azimio la Umoja huku akitoa kibao kuhusu mgombea urais Raila Odinga na mgmbea mwenza wake Martha Karua.

Katika kiao hicho anasema kwamba Maisha ya Wakenya yamo salama mikononi mwa wawili hao, kibao hicho alitoa baada ya Raila kumtaja Karua kama Mgombea Mwenza wake.

Ikumbukwe kwamba mwaka wa 2017 Ben Githae aliunga mkono chama cha kisiasa cha Jubilee kilichokuwa kinaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na naobu wake William Ruto.

Githae amekuwa akivuma mitandaoni kwa mambo kadha wa kadha.

Kulingana na Githae nabii hana heshima kwao, kwa hivyo ametabiri kuwa Raila na Karua watashinda katika uchaguzi ujao wa Agosti 9.

"Wapendwa, Sijawahi predict mshindi πŸ’ͺ🏽 akaanguka na ni kwa uwezo wa Mungu lakini nabii hana heshima kwao .... πŸ™πŸΌπŸ‡°πŸ‡ͺπŸ‡°πŸ‡ͺ," Aliandika Githae.