Makena Njeri afunguka kuhusu hatari ya kuwa mwanaharakati wa jamii ya LGBTQ

Muhtasari
  • Makena Njeri afunguka kuhusu hatari ya kuwa mwanaharakati wa jamii ya LGBTQ
Makena Njeri
Image: Studio

Mkurugenzi Mtendaji wa Bold Network Africa, Chris Makena Njeri, anasema kuwa harakati mara nyingi zimewaweka kwenye hatari.

Akiwa kwenye mahojiano maalum na Mpasho Makena alieleza sababu kuu ya kufungua kampuni yake, ambayo anasherehekea mwaka mmoja tanguu iifunguliwe.

Aidha mtangazaji huyo wa zamani wa BBC amesema kwamba kampuni hiyo imepitia changamoto lakini wamejitahidi kuwaelimisha watu hasa wenye jamii ya LGBTQ.

Huku akizungumzia kazi yake ya uhanarakati alisema kuwa umemuweka kwenye hatari.

"Uharakati umeniweka kwenye hatari nikifikiria juu yake. Lakini ni nini kingine tunachopaswa kufanya?" Makena aliuliza.

"Ni aidha niwe shupavu na kuendelea kuwa shupavu juu ya hilo, au nikate tamaa na kutoweka tu. Nikifanya hivyo(nitaacha), nitakuwa na athari gani kwa watu sio tu wakware bali hata vijana wanaotaka kuwa shupavu. katika chochote wanachosukuma?"

Makena alisema wanataka watu wakue wajasiri kwa kila hali. Hata hivyo, Makena alikiri kuwa wanaharakati wote wanaishi kwa hofu licha ya kuwa na ujasiri.

“Tunaelewa kuwa hii ndiyo kazi tunayotakiwa kuifanya na tunazungumza na Mungu wetu ili atulinde na kuendelea na kazi hiyo bila woga,” alisema Makena.

Makena alisema mara nyingi wamekabiliwa na ubaguzi, kukanyagwa na chuki kutoka kwa jamii.

"Siku zote huwa nabaguliwa. Kila nikiingia kwenye mitandao ya kijamii huwa nahukumiwa na kusahihishwa kuhusu kuwa mimi, hainisumbui tena kwa kuwa ni sehemu ya kazi ninayofanya.

Pia alisema kwamba haki inapaswa kutendeka kwa Sheilla Lumumba ambaye alibakwa na kuuwawa mwezi jana, kwani hadi leo hajaona haki ikitendeka licha ya mwenda zake kuwa mwanadamu kama yule mwingine.

Makena alikumbuka kanisa kwamba linapaswa kuhubiri upendo, na kutilia maanani kile wanachohubiri.