Afueni ya haraka!Mcheshi Akuku Danger alazwa hospitali tena

Muhtasari
  • Wakati huo, mcheshi huyo aliomba msaada kutoka kwa Wakenya na mashabiki ili kulipa bili ya hospitali
Image: INSTAGRAM// AKUKU DANGER

Mcheshi wa churchill Show Akuku Danger amelazwa hospitali tena.

Habari za kulazwa kwake zimetangaza na mwigizaji Sandra Dacha,haya yanajiri baada ya miezi 4 baada ya kulazwa hospital kwa muda huku akienda kwa koma.

Wakati huo, mcheshi huyo aliomba msaada kutoka kwa Wakenya na mashabiki ili kulipa bili ya hospitali.

Kupitia kwenye ukurasa wakke wa instagram Sandra amepakia picha ya mcheshi huyo na mashine akiwa hospitalini.

Haikusaidia kuzaliwa na sickle cell anemia kitu ambacho kinadhoofisha kinga yake.

Kulingana na Akuku, Sickle Cell Anemia haipewi kipaumbele na serikali ikilinganishwa na magonjwa mengine hatari kama saratani.

"Mimi naona huduma ya afya ni kitu kwa matajiri...tajiri wanaweza kupata dawa, matibabu, uchunguzi, dawa. Kwa watu masikini ni ngumu sana. Wagonjwa wa Sickle Cell wanahitaji dawa kila siku...na inagharimu pesa...kutokuwa na dawa ni hatari kwa afya yako," Akuku alibainisha.

Mashabiki wwamemtakia afueni ya haraka.KUtoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.