'Alikuwa anataka nimfungulie kampuni,'Anerlisa atoa sababu ya kuachwa na mmoja wa ex wake

Muhtasari
  • Anerlisa muigai ni miongoni mwa wajasirimali wanawake nchini ambao wamefanikiwa maishani kupitia bidii ya kazi yao
Anerlisa Muigai
Image: Anerlisa Muigai/INSTAGRAM

Anerlisa muigai ni miongoni mwa wajasirimali wanawake nchini ambao wamefanikiwa maishani kupitia bidii ya kazi yao.

Kwa mara ya kwanza Anerlisa amefichua sababu tano za kuachwa na ex wake, huku akiwashauri mashabiki kuhusu uhusiano wa kimapenzi na kile kinachohitajika.

Huku akiwashauri na kuwafichulia mashabiki wake sababu ambazo hufanya mahusiano mengi kuanguka alifichua sababu ya kumaliza mahusiano yake ya awali.

"Nimekuja kugundua sababu kwa nini mahusiano mengi ukamilika,kutokana na uzoefu wangu, kukosa heshima,kujiskia kuwa na haki kwa mambo ya mtu mwingine au maisha

Nilikuwa kwenye uhusiano ambapo mwenzi wangu alianza kuniambia nimwambie PIN ya ATM,wakati mwingine nikiongea na mama yangu anataka kujihusisha na mazungumzo yetu

Kuingia kwenye uhusiano kwa ajili ya sababu zako za ubinafsi,wacha nicheke mmoja wa ex wangu aliniuliza tumekuwa pamoja kwa mwaka mmoja kwa nini nisimsaidie kama vile kumjengea nyumba na hata kumfungulia kampuni kama yangu, nilimjibu ni kamwambia kama uliona kuanzisha uhusiano na mimi kutakutajirisha haya basi uko kwenye uhusiano ambao haufai

Niliachwa kabla ya wiki moja," Aliandika Anerlisa.

Aliendelea na ushauri wake na kusema jambo lingine ambalo linawafanya wapenzi kuachana ni kuwa na siri nyingi kwenye uhusiano.

Huku akisema hayo alifichua jinsi mmoja wa ex wake alitaka kumtapeli pesa.

"Kuwa na simu za siri na kutojua kile anachoendelea mpenzi wako,siku moja nilitoka kazi na nikafungua mlango wa moja ya majumba zangu na kuskiza jinsi mtu ambaye nilikuwa  namhumbia wakati huo alikuwa anapanga kunitapeli

Mtu ambaye alikuwa anazungumza naye alikuwa anamsaidia jinsi ya kupanga nilianza kurekodi mazungumzo yao, kiasi cha pesa ambacho walikuwa wamepanga ni dollar 30,000 lakni hawakufanikiwa."