'Naonekana kuwa mwanamke aliyetawanyika,'Akothee asema huku akimsifia mwanawe Vesha

Muhtasari
  • Akothee alimlimbikizia sifa Vesha na kufichua jinsi amekuwa guzo yake na rafiki wa karibu, na jinsi amekuwa akimpa mawaidha
Akothee na bintiye Vesha Okello
Akothee na bintiye Vesha Okello
Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Msanii na mjasirimali maarufu Esther Akoth, anayefahamika sana kwa jina la Akothee, ni mama mwenye furaha baada ya kusherehekea siku ya kuzaliwa na kifungua mimba wake.

Kulingana na ujumbe aliopakia kwenye ukurasa wake wa instagram Akothee,alimtakia Vesha heri njema ya siku yake ya kuzaliwa.

Akothee amesema kwamba amekuwa akionekana kama mwanamke aliyetawanyika kutokana na uhusiano wake wa awali usio faulu lakini licha ya hayo ni mama ambaye anajivunia Afrika.

Akothee alimlimbikizia sifa Vesha na kufichua jinsi amekuwa guzo yake na rafiki wa karibu, na jinsi amekuwa akimpa mawaidha.

"Jukumu langu linaanza na wewe, asante sana kwa kuweka kiwango cha juu kwa ndugu zako! Ingawa ninaonekana kama mwanamke aliyetawanyika kwa sababu ya uhusiano wangu uliofeli hapo awali, mimi ndiye mama mwenye Fahari zaidi katika Afrika

Ninajivunia Mafanikio yako 💪 wewe ni dada yangu wa pekee ambaye ninashiriki naye moyo wangu wa ndani. Ninapenda ustadi wako wa kufanya kazi

Ninapenda maoni ninayopata kutoka kwa kampuni unazofanyia kazi, Ooh Madam director you are the Best

Niruhusu niombe radhi hadharani ingawa tayari nilifanya hivyo nje ya kamera 💪 sikuwahi kutaka kukuacha uende 😭😭😭. Asante kidogo kwa ujasiri wako wa kuniambia kama ilivyo

"Mama Niruhusu niende kuwafanyia kazi watu wengine ili nipate Uzoefu zaidi na mtandao ili kusaidia biashara zetu vyema."