Wewe ni wa baraka-Betty Kyallo asherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe kwa ujumbe maalum

Muhtasari
  • Ni furaha ya kila mzazi kumuona mwanawe au wanawe wakikua kila kuchao, na hata kuendelea na maisha yao
Instagram, KWA HISANI
Instagram, KWA HISANI
Image: Betty Kyallo

Mwanahabari na mjasirimali Betty Kyallo sio mgeni vinywani mwa wengi au kwenye mitandao ya kijamii.

Betty amekuwa akifahamika sana kutokana na bidii ya kazzi yake, na kupiga hatua moja hadi nyingine ya maisha na biashara yake.

Pia anafahamika kutokana na uhusiano wake wa kimapenzi, amapo hajakuwa akificha uhusiano wake kutoka kwa mashabiki.

Ni furaha ya kila mzazi kumuona mwanawe au wanawe wakikua kila kuchao, na hata kuendelea na maisha yao.

Betty amebarikiwa na mtoto mmoja ambaye anaadhimisha miaka 8 hii leo,huku akiwa mwenye furaha alimlimbiikizia sifa teele mwanawe anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Kulingana na Betty mwanawe ni baraka kwake na kwa familia yake.

Pia alimtakia kila la kheri, na kumuomba Mungu amlinde katika maisha yake, na hatua anazozichukua kila siku.

"Binti yangu mpendwa Ivanna. Heri ya miaka 8 ya kuzaliwa. Unaleta furaha na furaha nyingi katika maisha yetu. Wewe ni baraka. Unapendwa sana nami, familia yako yote lakini jinsi inavyostaajabisha WEWE NI KIPENZI CHA MIUNGU. Nakupenda mpenzi. Umekusudiwa kwa kila kitu ambacho ni KUU! Niko hapa kukuona ukiangaza kila siku. Utakuwa na sherehe kubwa zaidi kwa sababu unastahili," Betty Aliandika.