Msanii Size 8 afichua kwa nini hataweza kupata mimba tena

Muhtasari
  • Msanii wa nyimbo za injili Size 8 akiwa kwenye mahojiano ameeleza kwa nini hataweza kuwa mjamzito au kubeba ujauzito tena

Msanii wa nyimbo za injili Size 8 akiwa kwenye mahojiano ameeleza kwa nini hataweza kuwa mjamzito au kubeba ujauzito tena.

Akizungumza katika mahojiano na Nicholas Kioko, Size 8 alisema kuwa kwa sasa anasumbuliwa na shinikizo la damu na anapokuwa mjamzito, shinikizo hupanda.

Size 8 alisema kuwa ni Mungu tu kwamba aliweza kuzaa watoto wake wawili. Alisema ujauzito wa Wambo na Junior nusura umuue kwa sababu alikuwa na shinikizo la juu la damu

Alieleza jinsi shinikizo lilisababisha kifo cha mtoto wake wa tatu na pia kuendelea na kufichua kwamba alikuwa karibu kufa mnamo Machi alipokimbizwa hospitalini kwa sababu shinikizo lake. ilikuwa juu sana sana.

Size 8 alihitimisha kwa kusema kuwa hataweza kuzaa tena.

Kwa sasa msanii huyo amebarikiwa na watoto wawili,ambao aliwapata kwa shida.

Pia akiwa kwenye mahojiano hayo aliwahimiza wakristo waweze kupendana kwani hata biblia inasema Mungu ni upendo, na kuwasaidia wanyonge hasa wakati huu maisha yamekuwa magumu.