logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Wewe ni sehemu ya hadithi yetu nzuri ya mapenzi" Musila amsherehekea mtangazaji aliyemuunganisha na Guardian Angel

Musila alisema kwamba haukuwa mpango wao kupendana na Guardian Anfel ila mapenzi yaliota siku waliyokutana.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri29 June 2022 - 14:15

Muhtasari


• "Umenifundisha jinsi ya kufurahia maisha bila msamaha na ninaamini mimi ni mwanafunzi wako mzuri" - Esther Musila kwa mtangazaji aliyemuunganisha na mumewe.

Esther Musila, mke wa mwimbaji wa miziki ya injili Guardian Angel amekuwa mtu wa hivi punde kumsherehekea mtangazaji maarufu Maina Kageni katika siku yake ya kuzaliwa.

Mwanamama  huyo mahusiano pamoja na ndoa yake na mwinjilisti Guardian Nagel viligonga vichwa vya habari mwishoni mwa mwaka jana kutokana na tofauti kubwa iliyopo baina ya umri wao, huku Musila akiwa na watoto ambao ni rika la mumewe, Guardian Angel.

Baadae katika mahojiano ya kipekee na wakuza maudhui, Musila alifunguka wazi alipopatana na mumewe wa ndoa, Guardian Angel na kulitaja jina la mtangazaji huyo pakubwa kuwa ndiye aliyekuwa kama daraja kuwapatanisha wawili hao ambao kwa sasa wanaishi kama mke na mume halali baada ya kufunga harusi ya faragha.

Na urafiki wao pamoja na shukurani zake za dhati kwa mtangazaji huyo zilidhihirika wazi wakati alipomwandikia ujumbe mzuri mtangazaji huyo huku akimshukuru kwa kumuunganisha na Guardian Angel.

Musila alimumiminia mtangazaji huyo maarufu sifa huku akimwita mtu wa maana sana kwake na kudokeza kwamba tarehe ambayo aliwakutanisha na Guardian Angel ambaye ni mume wake, mpango mzima haukuwa wawili hao kuwa na huba baina yao bali mapenzi yao yalianza kuota siku hiyo.

“Ulinitambulisha kwa mwanaume ambaye sasa ninamwita mume wangu, na ingawa huu haukuwa mpango wetu tulipokula chakula cha mchana tarehe 13.03.2020, naamini Mungu alikuwa na mipango yake mwenyewe, na wewe ni sehemu ya hadithi yetu nzuri ya mapenzi na nitafanya. daima kuwa na deni kwako. Umenifundisha jinsi ya kufurahia maisha bila msamaha na ninaamini mimi ni mwanafunzi wako mzuri,” Aliandika Musila kwenye Instagram yake.

Esther Musila pia alimtakia mtangazaji huyo kila la kheri katika siku hii ya kipekee ambapo alikuwa akisherehekea siku ya kuzaliwa, huku akimtsja kuwa baraka katika familia ya Omwaka – jina halisi la mumewe Guardian Angel.

“Mungu aendelee kukuongoza na kukulinda siku zote za maisha yako. Urafiki wenu una maana sana kwangu na kwetu akina Omwaka na mimi Looooove you biiiig time. Enjoy your day and week.!! Furaha na furaha njema siku ya kuzaliwa,” alimalizia Musila.

Ama kweli mapenzi ni kama magugu, huota katika udongo wowote!


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved