"Guchi ni 'special' kwangu," Stivo Simple Boy aeleza sababu ya kumlaki na maua JKIA

Guchi na Simple Boy wanatarajiwa kufanya tamasha pamoja wikendi hii.

Muhtasari

• Stivo Simple Boy alisema hana uhakika kama watafanya collabo lakini nafasi ikijitokeza na Guchi akubali, watafanya.

• Guchi watapanda jukwaa moja na Simple Boy katika tamasha wikendi hii nchini Kenya.

Msanii Guchi pamoja na Stivo Simple Boy
Msanii Guchi pamoja na Stivo Simple Boy
Image: Instagram

Msanii wa humu nchini StIvo Simple Boy amezungumzia kitendo chake cha kuelekea katika ang atua ya JKIA kumlaki msanii kutoka Nigeria, Guchi ambaye wikendi hii ako na tamasha kali nchini Kenya.

Msanii huyo ambaye alishangaza wengi kwani haijawahi tokea yeye kuonekana akihaha kweli kwenda uwanja wa ndege kumlaki mtu yeyote, tena na koja la maua ya kupendeza, na alipoulizwa kuhusu hilo na baadhi ya wale waliohisi pengine ana mahusiano naye, Simple Boy alisema kwamba amefanya hivo kwa sababu Guchi ni Rafiki yake mkubwa na pia kufichua kwamba watafanya tamasha hilo pamoja.

“Guchi ni wa kipekee, si mpenzi wangu lakini ni Rafiki yangu, Akiwaziri humu nchini kuna tamasha tutafanya na yeye na mashabiki watarajie mambo makubwa kutoka kwangu na Guchi,” alisema Stevo Simple Boy.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao ‘Freshi Barida’ alisema kwamba hana uhakika kama watafanya collabo pamoja na yeye lakini alisema kama Guchi atakubali bila shaka watafanya muziki pamoja.

Simple Boy alisema kwamba muziki wake uko tofauti kidogo na wasanii wengine kutokana na ukweli anaouimba kwenye mashairi yake na kusema kwamba ndicho chanzo kikubwa cha yeye kuteuliwa miongoni mwa wasanii wengi kuwa msanii wa kipekee kumlaki Guchi katika ang atua ya JKIA.

“Mimi ni mnyenyekevu na pia mimi napenda ukweli. Kama kitu ni mbaya mimi nakuambia ni mbaya na kama ni nzuri vile vile nakuambia hivo,” alisema Stevo Simple Boy.