logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee asema atazaa mtoto bila kushiriki kitendo "Nitaendea Artificial insemination Ufaransa"

"Ninachotaka ni mtoto wangu mwenyewe asiye na drama kabla nifike miaka 45. Nitawekewa mbegu za kiume" - Akothee

image
na Radio Jambo

Burudani08 July 2022 - 05:12

Muhtasari


• Msanii huyo alisema ana mapenzi ya dhati kwa watoto na ndio maana ameamua kutafuta mwingine tena.

Msanii na mjasiriamali Esther Akoth almaarufu Akothee

Msanii maarufu ambaye pia ni mmoja kati ya wajasiriamali weney mafanikio makubwa Afrika Mashariki, Akothee amezua gumzo tena kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufichua kwamba yupo nchini Ufaransa kwa ziara ya kutafuta mtoto mwingine.

Msanii huyo mama wa watoto watano wenye baba tofauti ameweka wazi kwamba safari hii hataki kuzaa mtoto na mwanaume yeyote kwa lengo la kuepuka drama za kusumbuana na baba mtoto bali analenga kuzaa mtoto wa kuwekea mbegu za kiume, almaarufu kwa lugha ya kimombo, ‘Insemination’

Alisema kwamba mapenzi yake kwa watoto hayawezi kupimika kwa mizani ya dunia hii wala kuonekana kwa darubini zozote humu ulimwenguni na kusema kwamba hisia zake bila mtoto zinamwendekeza kutafuta mmoja kabla ya miaka 45 kumfika.

“Nina kitu fulani tu na watoto. Nimekosa kitu na sitaki kupata ujauzito nikiwa na miaka 45, na kwa kuwa inaonekana wazi kwamba huenda sitapata mwenza hivi karibuni nimeamua kutafuta mtoto kwa njia mbadala,” aliandika Akothee kwenye Instagram yake.

Akothee aliwataka wambea kukaa mbali na yeye muda watakapomuona na mtoto kwani hatakuwa tayari kujibu maswali ya kipuuzi, ndio maana ameamua kuweka wazi kila kitu mapema.

“Nitaenda kwa Artificial insemination hapa Ufaransa. Kwa hiyo ukiniona nina mimba usiniulize baba ni nani. Ninachotaka ni mtoto wangu mwenyewe asiye na drama, fanya kile unachotaka kufanya katika maisha haya, ni maisha yako,” Akothee alimaliza kwa ushauri nasaha.

Siku za nyuma msanii huyo amewahi weka wazi kwamba kabla ya kufika miaka 45, atataka sana kupata mtoto mmoja wa mwisho. Pia alisema akifika umri huo rasmi atastaafu kutoka maisha ya umaarufu mitandaoni.

Huyu si msanii wa kwanza kutafuta mtoto kwa njiqa hiyo kwani juzi msanii wa bongo fleva, Malkia Karen aliweka wazi kwamba mwanawe alimpata kwa njia hiyo ya kuwekewa mbegu za kiume kwa kile alisema kwamba alikuwa na uhitaji wa mtoto pasi na kuona mwanaume bora wa kuzaa naye, kupelekea yeye kununua mbegu za kiume hospitalini zinakohifadhiwa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved