"Sijui niandae party ya kuchipuka kwa jino la kwanza la mwanangu" - Vera Sidika

Mwanasosholaiti huyo pia alisema mwanawe ameqanza kutamka 'kaka' sana huenda kakake yuko njiani.

Muhtasari

• Vera Sidika alidokeza kuhusu uwezekano wa kuandaa hafla ya kusherehekea kuchipuka kwa jino la kwanza la Asia Brown.

Asia Brown, Mwanawe Vera Sidika na Brown Mauzo
Asia Brown, Mwanawe Vera Sidika na Brown Mauzo
Image: Instagram screenshot

Mwanamitindo Vera Sidika ameibuka na jingine tena baada ya kudai kwamba huenda ataandaa hafla kubwa ya kusherehekea kuchipuka kwa jino la kwanza la mwanawe Asia Brown.

Kupitia kwa Instagram yake, Vera Sidika alisema kwamba kulingana na dalili zote, huenda mwanawe Asia akachipukiza jino la kwanza siku yoyote kuanzia sasa na kudokeza kwamba huenda hafla ya kusherehekea juhudi hizo za jino la kwanza kuonekana.

“Ninaapa jina la kwanza la Asia linataka kuchipuka, nina furaha, sijui tena turushe hafla ya kusherehekea hili,” aliandika kwenye instastories zake.

Kama kawaida wambea wenye chuki walijumuika pale ambapo wengi walimsema kwamba ana pesa za kuharibu kwa mambo yasiyo na maana huku wengine wakimuita kwa maneno mazito.

Ikumbukwe hivi majuzi mwanasosholaiti huyo pamoja na mchumba wake Brown Mauzo waliandaa hafla kubwa ya kifahari kusherehekea nusu mwaka, yaani miezi sita tangu kuzaliwa kwa mwanao ambapo Mauzo alimsihi Sidika kumpa watoto wengine zaidi.

Sidika katika msururu wa instastories zake alidokeza kwamba pengine huenda watazaa mtoto mwingine tena ambaye labda safari hii atakuwa wa kiume. Alidokeza haya akisema kwamba Asia ameanza kutaka kutamka neno ‘kaka’ sana.

“Ooh mwana, inaonekana kama Asia anataka kuanza kuzungumza. Lakini mbona anatamka ‘kaka’ sana, ni kama kakake ako njiani?” Sidika aliandika.

Hivi majuzi Vera Sidika alifichua kwamba pindi atakapomalizana na masuala ya kulea watoto basi atahitaji kufanya upasuaji wa matiti ili kuyafanya maziwa yake kuwa yenye muonekano wa mviringo, na kudokeza kwamba suala la kuwa mwanasosholaiti bado litazidi kwani yeye bado atazidi kuwa na mwonekano wa kifahari hata baada ya kuwa mama.

Vera Sidika na Brown Mauzo waliweka mahusiano yao wazi mwaka wa 2020 ambapo wengi walikisia kuwa watabwagana baada ya muda mfupi ila wao wamedhibitisha vinginevyo kwa kudumu katika mahusiano zaidi ya miaka miwili na mtoto juu.

Hongera kwao!