(Video) Jimal asherehekea siku ya kuzaliwa ya 'rafiki' yake Wangari, mkao wao wazua umbea mtandaoni

Jimal aliachana na wake zake wote Amira na Amber Ray mwishoni mwa mwaka jana.

Muhtasari

• Mfanyabiashara huyo alisema kwamba hana haja ya mapenzi na fikira zake sasa ni kutafuta pesa.

Mfanyibiashara maarufu kwenye sekta ya matatu humu nchini Jimal Roho Safi amepakia video kwenye TikTok yake akimsherehekea Rafiki yake wa karibu Wangari Thiong’o siku yake ya kuzaliwa.

Kwenye video hiyo ambayo marafiki hao wawili wanaonekana kukete mkabala, wanaonekana wakipiga ‘cheers’ ya vinywaji huku ngoma Lover Boy yake msanii Barnaba Classic ikiimba kwa maudhui kwamba maisha si lazima kuchumbiana.

“Furaha zaidi ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yangu bora, endelea kuwa mtu wa kushangaza kama wewe. @wangari_thiongo,” alifuatisha ujumbe huo Jimal Rohosafi.

Mjasiriamali huyo amekuwa akizua gumzo mitandaoni haswa kutokana na kile anachoita ‘urafiki bora wa karibu’ na mwanadada huyo ambaye ni mwanafasheni wa urembo, ambapo wengi wamekuwa wqakizua uvumi mitandaoni kwamba wawili hao huenda wakaishia kwenye mahusiano ya kimapenzi ila tu pengine ni muda haujafika wa kuyaweka wazi lakini Jimal amekuwa akisisitiza hakuna kingine baina yao zaidi ya urafiki tu.

Jimal aliachana na wanawake wake wawili mwaka jana katika Sakata lililojawa manejno ya kashfa mitandaoni huku wanawake hao wote wakirushiana maneno makali tena ya nguoni.

Mke wa kwanza, Amira ndiye alikuwa wa kwanza kubwaga manyanga na kumuondokea mwanamitindo Amber Ray ambaye alikuwa kama nyumba ndogo ila naye Jimal akamshinda miezi michache baadae na kumbwaga hadharani alipopakia video kwenye Instagram yake akiifuta tattoo aliyokuwa amechora mgongoni ya mfanyibiashara huyo kama ishara ya mapenzi.

Tangu kuachana kwao miezi kidhaa iliyopita, Jimal alidokeza kwamab angechukua likizo ndefu kutoka uwanja wa mapenzi na kusema kwamba sasa fikira zake sasa ni kutafuta pesa.