"Bahati ajue siasa si kama kanisa, kama amepigwa, apigane pia, asikuwe analialia" - Ringtone

Ringtone alikuwa anatoa ushauri kwa msanii bahati ambaye ameingia kwenye siasa.

Muhtasari

• “Mimi nataka kumuambia Bahati ajue siasa si kanisa, siasa si muskiti, siasa si harusi. Siasa ni pahali pa kupigana" - Ringtone.

Wasanii Ringtone na Bahati
Wasanii Ringtone na Bahati
Image: RINGTONE, BAHATI (Instagram, YouTube screenshot)

Ringtone, ambaye hatimaye ameamua kuwafuata wenzake bahati Kioko na Willy Paul kwenye miziki ya kidunia baada ya kuigura tasnia ya injili, sasa anatetea kilio alichokitoa mahakamani wakati anatoa Ushahidi dhidi ya mwanablogu Robert Alai ambaye alimpiga rungu ya kichwa mwaka jana katika barabara moja mtaani Kilimani, Nairobi.

Ringtone alijitetea kwa kusema kwamba yeye analia mara moja moja tu hali ya kuwa msanii Bahati huwa na mazoea ya kulia kila mara kama mtoto.

Bahati amekuwa akionekana katika matukio mbali mbali akitokwa na machozi tu, tukio la hivi karibuni likiwa ni lile pindi baada ya kushinda tikiti ya Jubilee kuwania ubunge Matahre lakini akanyimwa tikiti ile baada ya Jubilee kusema kwamba muungano wa Azimio-One Kenya ambao chama hicho ni mojawapo, wameafikiana kufanya kitu kinaitwa ‘zoning’ ili kuwaondoa wagombea wasiokuwa na nguvu na kuwaunga mkono wagombea wenye ushawishi mkubwa.

Bahati alilia hadharani tena mbele ya kamera za wanahabari huku akiteta kwamab amefanyiwa hujuma baada ya kutumia pesa na nguvu nyingi kufanya kampeni.

Ringtone ambaye amejiunga nao kwenye uwanja wa miziki ya kidunia sasa ametoa ushauri kwa Bahati huku akimwambia kwamba ni sharti ajue siasa si kama Sanaa ya injili. Ikumbukwe Ringtone aliwahi jaribu siasa mwaka wa 2012 ambapo aliwania ubunge Kitutu Masaba katika uchaguzi wa mpito lakini akashindwa na kuburura mkia.

“Mimi nataka kumuambia Bahati ajue siasa si kanisa, siasa si muskiti, siasa si harusi. Siasa ni pahali pa kupigana. Siasa inakuwa ni nani alipiga mwingine. Sasa kama yeye amepigwa juzi, na yeye aende ampige yule aliyempiga, lakini isiwe si ile kumpiga ya kuumiza,” alitoa ushauri Ringtone.

Ringtone alisisitiza kwamba kwa kupiga hana maana ya vita bali ile kuweka watu wake pamoja ili kupiga kelele kwa kutamka jina lake na kumshinda mpinzani wake mwenye alikuwa na wafuasi wengi waliompigia kelele.

Ringtone alisema kwamab yeye aliamua kutumikia Wakenya wote badala ya kugombea kiti cha ubunge kwa sababu nafasi hiyo inakufunga kwa eneo moja tu lakini kwa muziki ni Wakenya wote wanaufikia muziki huo.