(+Picha) "Ahsante kwa kunipa mapenzi ya baba ambayo sikuwahi pata awali" msichana amwandikia Sakaja

Msichana huyo ni yule ambaye Sakaja alijitolea kufadhili elimu yake kwa kumlipia karo shule ya upili

Muhtasari

• Msichana ambaye Sakaja alifadhili elimu yake alimwandikia barua ya kumsherehekea na kumwombea awe gavana.

• Alimshukuru Sakaja kwa kumkubalia kuwa mmoja wa familia yake na kumpa mapenzi ya baba ambayo hakuwa nayo.

SAeneta wa Nairobi Johnson Sakaja na mwanafunzi aliyefadhili elimu yake
SAeneta wa Nairobi Johnson Sakaja na mwanafunzi aliyefadhili elimu yake
Image: Johnson Sakaja (Facebook)

Msichana mmoja amemtungia barua ya yenye shukrani kochokocho seneta wa Nairobi Johnson Sakaja huku akimshukuru kwa hatua ya seneta huyo kufadhili elimu yake ya shule ya upili.

Msichana huyo ambaye bado jina lake Sakaja hakuliwahi liweka hadharani kwa umma aliandikia barua Sakaja huku akimtaja kuwa baba mwema kabisa kote duniani kwa hatua yake ya ihsan ya kumlipia karo ya shule huku akiahidi kutia bidii na kuboresha matokeo yake hata zaidi ya yale ya muhula uliopita.

Kupitia barua hiyo ambayo Sakaja aliipakia kwenye ukurasa wake wa Facebook, binti huyo anaonekana akimsifia na kumshukuru Sakaja pakubwa, barua ambayo Sakaja alisema ilimgusa pakubwa na kumpa motisha wa kuendelea kuwasaidia wengine wenye hali kama ya binti huyo.

“Pokea barua hii kutoka kwa binti yako, ninakushukuru kwa yote mazuri ambayo umenitendea. Umenifanya kuwa binti mwenye furaha na kuwa mmoja wa wanafamilia yako, wewe ni baba mzuri kupindukia. Ninakushukuru sana juhudi zako na pia kwa kunipa mapenzi ya baba ambayo sikuwahi kuyapata awali,” binti huyo alimuandikia barua nzuri ajabu.

Pia binti huyo alidokeza kwamab muhula uliopota hakufanya vizuri vile lakini akaahidi seneta Sakaja kwamba katika mihula ijayo atatia fora zaidi ili kumuonesha kwamab msaada wake haujaenda na maji.

Msichana huyo amemuomba Sakaja kukutana naye kabla ya kurejeaq shuleni Jumatatu.

“Baba, ningependa sana kukutana nawe kabla ya kurejea shuleni Jumatatu. Mimi na familia yangu ambayo tunaishi nayo tunakuombea usiku na mchana ili uwe gavana na kiongozi wetu. Ahsante kwa kila kitu,” msichana huyo aliandika.

Maneno haya yalimfikia Sakaja kwa hamu kubwa ambapo alisema yamemgusa mno na kumpa motisha zaidi ya kuzidi kutenda mema kwa watu wenye mapungufu mbali mbali.

“Hii inanifanya niendelee. Kwa wadogo zangu wote ambao tunawasaidia kupitia shule, mnanitia moyo nisikate tamaa. Tutafanikiwa. Sitawahi kuwaacha. Nawapenda nyote,” Sakaja aliandika.