"Kutafuta umaarufu mitandaoni hautakupa pesa, utakupa tu ngono ya bure, vyakula ghali" - Akothee

“Mitandao ya kijamii ni utapeli mkubwa, kuwa makini na mtu unayemfuata kwenye mitandao" - Akothee

Muhtasari

• “Chochote unachokifanya sasa kitaonekana katika maisha yako ya mbeleni, sasa toka kwenye mitandao ya kijami" - Akothee

msanii Esther Akoth
msanii Esther Akoth
Image: Facebook

Msanii Akothee katika siku za hivi karibuni ameonekana ni mtu mwenye kutema lulu sana mitandaoni huku akitoa ushauri bila malipo kwa wafuasi wake.

Kastika msururu wa jumbe za ushauri ambazo amekuwa akipakia kwenye mitandao yake, Akothee anawaambia watu kwamba ni sharti wawe katika usukani kuratibu mwelekeo wa maisha yao wenyewe pasi na kutegemea mtu.

Akipakia picha za jumba lake la kifahari ambalo amelijenga kijijini mwao kama sehemu ya kujiandaa katika maisha yake ya kustaafu pindi atakapofikisha miaka 45, kuacha muziki na kuondoka kwenye mitandao ya kijamii, Akothee alishauri kwamba chenye unafanya leo kitakuja kuonekana katika maisha yako ya mbeleni.

“Chochote unachokifanya sasa kitaonekana katika maisha yako ya mbeleni, sasa toka kwenye mitandao ya kijamii na uache kujilinganisha na ukurasa wa 20 wa mtu. Jiulize unataka kuwa wapi miaka 10 ijayo,” aliwashauri wafuasi wake.

Akijitolea mfano, Akothee alisema yeye ana miaka 41 lakini alianza kujenga kasri lake akiwa na miaka 14 tu na kusema kwamab yeye ndiye mwanamke wa kipekee anayetoa ushauri mzuri huku akiwataka watu kuwa makini na wanawake wanaowafuatilia mitandaoni kama kweli wanatoa motisha ama wanakandamiza nyoyo zao.

“Mitandao ya kijamii ni utapeli mkubwa, kuwa makini na mtu unayemfuata kwenye mitandao, kaam wanakupa motisha, wanakuhimiza ama wanakukandamiza na ndoto za maisha yako na kukufanya uhisi kama huna uhai wala nafasi katika dunia hii ya viumbe hai,” alisema Akothee kupitia Facebook yake.

Akionekana pia kugusia wale wenye kupenda vya bwerere, alishauri kwamba kupata kitu kilicho chako cha halali ni sharti mtu ufanye juhudi za kweli na kusema kwamba umaarufu katika mitandao kitu tu utakusaidia ni kuingia katika migahawa mikubwa, kupata ngono ya bure na kula vyakula ghali.

“Rafiki yangu ni lazima utie bidi sana ili kuwa na maisha mazuri, vitu vizuri huja na kujitolea muhanga, katu haviji na Iphone, na picha zilizohaririwa na mazingira yasiyo ya kweli. Huwezi pat ahata shilingi moja kwa kuwa maarufu, umaarufu utakufanikishia tu kuingia kwenye mahoteli ya kifahari, ngono ya bure na vyakula vya bure pia,” Akothee alitema moto wa busara.